Meneja
wa Kinywaji cha Redds, Victoria Kimaro akizungumza na Waandishi wa
Habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam
jana wakati wa kutangaza zawadi ya Mshindi wa Taji la Reddds Miss
Tanzania 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency,waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
………………………………………………..
Akizungumza na waandishi wa
Habari Jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa kampuni ya LINO AGENCY Hashim
Lundenga alisema katika fainali za shindano la Redds Miss Tanzania 2012
zitafanyika tarehe 3 Novemba 2012 katika ukumbi wa Blue Pearl Hotel,
(Ubungo Plaza) jijini Dar es salaam ambapo ni shindano linaloshirikisha
washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
Leo hii tunapenda kuchukua
nafasi hii kuwatangazia rasmi kuwa katika fainali ya Redds Miss Tanzania
mwaka zawadi zitakuwa kama ifuatavyo
1) Mshindi wa Kwanza atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 8,000,000/- pamoja na gari
2) Mshindi wa pili atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 6,200,000/-
3) Mshindi wa tatu atapata zawadi ya pesa taslmu shs: 4,000,000/-
4) Mshindi wa nne atapata zawadi ya pesa taslimu shs; 3,000,000/-
5) Mshindi wa tano atapata zawadi ya pesa taslimu shs: 2,400,000/-
6) Mshindi wa sita hadi wa 15 kila mmoja atapata shs: 1,200,000/-
7) Washiriki wengine wote waliobaki kila mmoja atalipwa shs: 700,000/-
Katika shindano hilo ambalo
ndani yake kuna mashindano mengine madogo [Fast Tract] tayari washiriki 3
wameshajipatia tiketi ya kuingia katika [Top 15 Finalist]
Washiriki hao ni Lucy Stephano – Miss Photogenic
Magdalena Roy – Top Model
Mary Chizi – Top Sport Woman
Shindano dogo lingine limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 26 Oktoba 2012 la kumtafuta mrembo wenye Kipaji. Miss Talent.
Na tarehe 28 Oktoba 2012 atapatikana Miss Personality.
Nae Meneja wa kinywaji cha Redds
Original Bi Victoria Kimaro amesema huu ni wakati sahihi wa kumpata
mshindi biomba mwenye vigezo sahihi hivyo kuwataka wapenzi wote wa
tasnia ya urembo na wapenda maendeleo kote nchini kujianda kupata tiketi
za kushudia fainali hiyo mapema ili kuweza kupata fursa ya kupata
burudani mbalimbali.Kwa kweli shindano la mwaka huu tunatarajia kuwa
litafana sana hasa kwa kuzingatia kuwa maandalizi yote yameshakamilika
kwa kiwango kikubwa na sisi kama wadhamini wakuu tunahakikisha kuwa
mwaka huu kila atakaefika kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza atakuwa na jambo
la kusimulia kwa sababu ni shindano la kipekee.
EmoticonEmoticon