Mary Gannon, amejiriwa kama mwalimu wa shule ya msingi kwenye shule ya Lakewood iliyopo Ohio nchini Marekani.
Tofauti na walimu wenzake, Mary anatumia miguu kuandika ubaoni na pia anatumia miguu kuandaa ripoti kwenye computer akitumia vidole vya miguu yake kuandika kwa kutumia keyboard ya kompyuta yake ya ofisini.
Mwalimu Mary ambaye hufundisha somo la hisabati na sayansi alizaliwa nchini Mexico akiwa hana mikono na alilewa kwenye kituo cha kulea yatima mpaka familia moja ya nchini Marekani ilipojitolea kumchukua na kumlea.
Mary alianza kazi kwenye shule hiyo mwaka jana kama mwalimu wa akiba lakini hivi sasa amejiriwa kabisa akifundisha wanafunzi wa darasa la saba na la nane,
Mbali ya kutumia miguu yake kufundishia, Mary pia anaendesha gari lake kwa kutumia miguu.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon