Watu watatu wa familia moja wanashikiliwa na polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kumuua kikongwe wa miaka 90 ili warithi mali zake
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea huko katika kijiji cha Ziga Wilayani Igunga mkoani Tabora jana
Kikongwe huyo ametambulika kwa jina la Mashiku Sepeta [90] ambaye alidaiwa hakuwa na watoto wa kuzaa mwenyewe
Polisi mkoani humo imesema kuwa, watu hao walikuwa na uroho wa mali kwani mzee huyo alijaaliwa kuwa na utajiri wa ng’ombe wengi hivyo waliona baadae huenda kungetokea ukorofi na kuamua kummalizia
Polisi imesema watu hao wanashikiliwa na polisi na kuwataja watuhumiwa hao kuwa ni Chenzega [30], Alli [40] na mwenzao mmoja
EmoticonEmoticon