MKUTANO WA WANAWAKE WAFANYABIASHARA

 Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami (kulia) akiongea na waandishi  wa habari jana(leo) jijini Dar es salam juu ya Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi ya Mashariki mwa Afrika unaofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza na unaotarajiwa kufunguliwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Mohamed Gharib Bilal  . Kushoto ni Makamu wa Mwenyekiti wa TWCC Anna Matinde. Mkutano huo unafunguliwa tarehe 22.10.2012 katika Hotel Kunduchi Beach.

Picha na MAELEZO_ Dar es salaam

Dkt.Bilal Kufungua Mkutano Wa Wafanyabiashara Wanawake

Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam 20.10.2012
 Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Wanawake wafanyabiashara wa Nchi ya Mashariki mwa Afrika unaonza kesho jijini Dar es salaam kwa lengo la kuimarisha mtandao wao. Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Tanzania Women Chamber of Commerce (TWCC) Fatma Riyami wakati akiongea na waandishi wa habari Ofisi kwake. Amesema kuwa Mkutano huo ambao ni wa saba(7) unafanyika nchini Tanzania kwa mara ya kwanza tangu walipoanzisha ushirikiano huo wa wanawake wafanyabiashara kwa nchi za Afrika Mashariki. Mwenyekiti huyo amesema kuwa wajumbe wa Mkutano huo wanatarajiwa kutoka katika Nchi za Kenya, Uganda, Rwanda , Burundi, Ethiopia , Sudan Kusini na mwenyeji Tanzania. Amesema kuwa Mkutano huo utakuwa fursa nzuri kwa wajumbe kutoka nchi zote saba kubadilishana uzoefu katika kazi ya kuwainua kiuchumi wakimama na kuimarisha Mtandao wa Wafanyabiashara wanawake katika Nchi za Afrika Mashariki. Ameongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kufanya soko la wafanyabiasha wanawake wa Afrika Mashariki kuwa kubwa na hivyo kuwainua kiuchumi wakimama. Aidha Bibi Fatma Riyami amesema kuwa TWCC imeanzisha matawi katika Mikoa ya Kagera, Mwanza, Pwani, Dodoma, Mbeya, Dar es salaam na Arusha ikiwa na lengo la kutaka kuwa karibu na wafanfanyabiashara wanawake kwa nia kuimarisha Umoja wao. Wakati huo Mwenyekiti huyo amewasisitiza wajumbe wa Mkutano huo kufika katika Hoteli hiyo ifikapo saa 1.30 Asubuhi , Mgeni rasmi atafungua mkutano huo saa 2.00 kamili

Bandari Makao Makuu Waibuka Washindi




Bandari Dar Mabingwa Inter-Ports Games

• Yang’ara na kuibuka na vikombe vingi


Bandari ya Dar es Salaam imeibuka na ushindi wa jumla katika michezo ya inter-ports games ambayo imefanyika jijini Mwanza hivi karibuni na kufungwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mh. Baraka Konisaga. Michezo hiyo imefanyika jijini huko kwa muda wa siku tano ambapo zaidi ya wanamichezo 400 wafanyakazi wa Bandari walishiriki michezo mbalimbali kama vile mpira wa miguu, pete, kikapu, riadha, bao na kuvuta kamba.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vikombe na zawadi nyingine kwa wanamichezo hao, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana aliwaasa wanabandari kuendelea kushiriki michezo kwa ajili ya kujenga afya zao lakini kubwa zaidi kutekeleza majukumu yao ya kila siiku kwa ufanisi. “Leo isiwe mwisho wa kushiriki michezo endeleeni kushiriki ili kuoboresha afya zenu lakini pia niwashauri kutekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na mkumbuke kwamba mmepewa dhamana kubwa na taifa lenu hivyo ni wajibu wenu kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa,” amesema Konisaga.

Katika michezo hiyo Bandari ya Dar es Salaam iliibuka na vikombe vingi zaidi ambapo katika mpira wa soka waliibuka washindi wa kwanza kwa kujinyakulia alama nyingi huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Makao Makuu.

Kwa upande wa mpira wa pete mshindi ni Bandari ya Dar es Salaam na nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bandari ya Tanga. Katika mchezo wa kikapu nafasi ya kwanza ilikwenda Makao Makuu wakati Bandari Tanga wakinyakua nafasi ya pili. Nafasi ya kwanza ya mchezo wa kuvuta kamba wanaume ilikwenda kwa Bandari ya Dar es

Salaam na nafasi ya pili ilinyakuliwa na Bandari ya Tanga.nafasi ya kwanza ilikwenda kwa Bandari ya Dar es Salaam na Bandari ya Tanga ilishika nafasi ya pili.

Kwa upande wa riadha Bandari ya Dar es Salaam iliibuka tena kidedea huku Bandari ya Tanga ikishika nafasi ya pili. Kwa upande wa wakimbiaji mita mia moja kwa wanawake medali ya dhahabu ilikwenda kwa mkimbiaji kutoka Makao Makuu, medali ya fedha ilikwenda kwa mkimbiaji wa Bandari ya Tanga na mshindi wa tatu alikuwa mkibiaji kutoka Bandari ya Dar es Salaam aliyeibuka na medali ya shaba.

Kwa upande wa wakimbiaji wa mita mia moja wanaume medali ya dhahabu ilichukuliwa na mkimbiaji wa Bandari ya Dar es Salaam, fedha mkimbiaji wa Bandari ya Dar es Salaam na shaba ilikwenda kwa mkimbiaji kutoka Bandari za Maziwa (Mwanza, Kigoma na Kyela). Kwa upande wa mita mia nne wanawake dhabau ilikwenda Bandari ya Dar es Salaam, fedha ilikwenda Bandari ya Dar es Salaam na shaba ilikwenda kwa mkimbiaji wa Makao Makuu. Kwa upande wa mita mia nne wanaume dhahabu ilikwenda Tanga, fedha ilikwenda Makao Makuu na shaba ilinyakuliwa na Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa upande wa mchezo mkongwe na wa jadi maarufu kama bao, Bandari ya Dar es Salaam iliibuka tena na ushindi wakati nafasi ya pili ilikwenda kwa Bandari ya Tanga. Kwa upande wa wachezaji bora wa kila mchezo, mlinda mlango mahiri wa timu ya Mtwara, Douglas Bahati aliibuka mshindi. Kwa upande wa mchezo wa mpira wa pete, Matalena Mhagama ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa aliibuka kidedea na nafasi ya kwanza. Kwa upande wa timu bora ya kuvuta kamba

Makao Makuu waliibuka na ushindi huku Bandari ya Mtwara ikiibuka na ushindi wa timu bora yakuvuta kamba wanaume. Mchezaji bora wa riadha ni Lucy Kyoma kutoka Bandari ya Dar es Salaam. Bandari zilizoshiriki katika michezo hiyo ni pamoja na Bandari Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza, Kyela, Kigoma na Makao Makuu yenyewe. Michezo hiyo hufanyika mara moja kila mwaka kwa kuwashirikisha wanabandari na hufanyika mara moja kwa kila kituo.
Previous
Next Post »