Mdahalo kuhusu sera ya kigeni Marekani


Rais wa Marekani Barack Obama na mpinzani wake wa Republican Mitt Romney wametofautiana kuhusu sera ya kigeni ya Marekani katika mdahalo wao wa mwisho wa runinga kabla ya uchaguzi ujao wa Urais.

Romney alimlaumu Rais Obama kwa kushindwa kutoa uongozi unaofaa kwa dunia na ameruhusu amani mashariki ya kati kuvurugika.

Hata hivyo Obama alimkosoa Romney akisema amekuwa akipinga sera zote kuu za marekani ikijumuisha kuivamia Iraq.

Wagombea hao wamezungumzia sana kuhusu swala tete la harakati za mageuzi katika nchi za kiarabu,sawa tete la ran, Israel na China.

Bwana Obama alisema mpinzani wake hana uelewa kuhusu sera ya kigeni lakini Romney naye akamwambia kuwa ameruhusu vurugu kukumba Mashariki ya kati.

 
Wagombea Mit Romney na Barack Obama wakielezea sera zao za kigeni

Kura za maoni zilizotolewa punde baada ya kukamilika mjadala huo, zilionyesha Obama kuwa mshindi.

Mjadala huo uliofanyika katika chuo kikuu cha Boca Raton, haukuwa na ubishi kama mjadala wa pili wiki jana ambapo rais Obama alijitokeza kisabuni kuonyesha wapiga kura kuwa ye ndiye kiongozi anayestahili kuchaguliwa mwaka ujao.

Lakini ubishi ulijitokeza mara kwa mara hasa ambapo Obama alitaka kuonyesha wapiga kura kuwa Mit Romney hana uelewa mzuri kuhusu sera ya kigeni na kwamba hawezi kuwa kiongozi mzuri.
Previous
Next Post »