12 wateketea hospitalini Taiwan


 
Moto uliozuka mapema leo asubuhi katika hospitali moja Kusini mwa Taiwan, imewaua watu 12 na kuwajeruhi wengine 60

Moto huo uliteketeza makao ya wazee yaliyowahifadhi wazee wagonjwa ndani ya hospitali hiyo mjini Tainan.
    
Afisaa mmoja wa hospitali hiyo, alisema kuwa waathiriwa walifariki kutokana na moshi mwingi. Wale waliojeruhiwa wanapokea matibabu katika hospitali kadhaa.

Hata hivyo kilichosababisha mto huo bado hakijajulikani.

Hospitali hiyo ilikuwa na wagonjwa zaidi ya 100 wengi ambao hawakuwa na uwezo wa kutembea bila usaidizi

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 94 ambaye alilazimika kutumia kiti cha magurudumu,kuukimbia moto huo na kujificha katika ghorofa ya poli.

Magari thelathini ya wazima moto yalifika katika hospitali hiyo na kupambana na moto hadi majira ya asubuhi dakika arobaini na tano baada ya kuzuka kwa moto huo.

Meya wa Taiwan, Lai Ching-te, alisema kuwa eneo ambako hospitali hiyo ipo pamoja na hali ya wagonjwa ndiyo ilikuwa changamoto kubwa kwa juhudi za kuokoa watu na kujaribu kuuzima moto huo.

Kulingana na mwandishi wa BBC , Wazima moto, waliwasili katika eneo la moto dakika kumi baada ya kuzuka kwa moto huo ingawa kwa sababu ya idadi kubwa ya wagonjwa , wenyeji walilazimika kuomba usafiri ili kuwapeleka wagonjwa katika hospitali zengine.

Moto huo unaaminika kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea katika mji mkuu wa Taiwan, katika miaka ya hivi karibuni.
Previous
Next Post »