Maoni kupata Katiba Mpya Mkoani Rukwa Hoja Ya Dini Yatawala

Mwananchi wa sumbawanga akitoa maoni juu ya katiba mpya katika viwanja vya maktaba ya mkoa wa Rukwa leo
Wananchi wa sumbawanga leo wamepata nafasi ya kutoa maoni kuhusu mchakato wa kupata katiba mpya,mbele ya wajumbe wa tume ya katiba, wananchi wamepata fursa ya kuchangia yale wanayodhani yanafaa kuwemo katika katibu mpya.
Wapo waliochangia kwa kuongea pia wapo waliochangia kwa njia ya maandishi 
Jambo Kubwa  ambalo limejitokeza katika mchakati huo ni suala la dini wengi watoa maoni wamekuwa wakizungumzia suala la dini , mfano mtu mmoja alisema angependa kwenye katiba ingeonyesha kuwa siku ya kuabudu waislamu ijumaa kuwa ni  siku ya mapumziko kama ilivyo siku ya jumapili kwa wakristo.

Mama mmoja aliyejitambulisha kuwa ni mwalimu yeye alisema kama waislamu wanataka kuwepo na mahakama yao hivyo haina budi na wakristo nao wapewe mahakama yao mama huyo aliweza kumnukuu baba wa taifa akisema "Mwalimu Nyerere alisema serikani haina dini" hivyo akahoji kama waislamu wakitaka mahakama yao serikari itakuwa na dini moja hayo ni baadhi ya maoni ya mama huyo 
Kama hiyo haitoshi nimeweza kuzungukia baadhi ya vijiwe vilivyo katikati ya mji wa sumbawanga ikiwa ni pamoja na soko la mitumba lililo jirani na uwanja wa kumbukumbu ya Nelson Mandela jirani na njia ya kwenda mkoa wa katavi nako huko hoja inayotawala ni suala la dini.
Je mwananchi mtanzania mzalendo unaona mchakato huu ukiegemea kwenye hoja ya dini na si mambo mengine tutapata katiba tunayoitataka?.
Mkami Jr
Mjengwa Blog -Sumbawanga
Previous
Next Post »