Aliyekojolea Quruan, waliochoma kanisa Kortini

KIJANA Emmanuel Josephat aliyedaiwa kukojolea kitabu cha Kuruan eneo la Mbagala amefikishwa katika Mahakama ya watoto kujibu mashitaka yake yanayomkabili
  Mbali na huyo pia Watu zaidi ya 3o wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka 20 na kusomewa mashitaka yao katika mahakama hiyo

Mashitaka hayo yakiwemo ya kuharibu kanisa, kuchoma moto ikiwemo na unyang'anyi wa kutumia silaha

Washitakiwa hao waliopandiwha katika kesi nnne tofauti walisomewa mashitaka yao na Wakili wa Serikali Mwandamizi Tumaini Kweka mbele ya Hakimu Sundi Kifimbo wa Mahakama hiyo

Kweka alidai Mahakamani hapo kuwa, kati ya Oktoba 10 na 12 mwaka huu, huko eneo la Mbagala washitakiwa hao kwa pamoja walikula njama na kuharibu mali mbalimbali za Kanisa la KKKT

Amedai mbali na kuharibu kanisa pia walifanya makosa mbalimbali ya unyang'anyi wa kutumia silaha na kudaiwa mahakamani hapo kuwa thamani zilizoibiwa na kuharibiwa zilikuwa na thamani ya shilingi Milioni 700

Hata hivyo washitakiwa wote walipotakwia kujibu mashitaka yao walikana mashitaka hayo na walirudishwa rumande kwa kukosa dhamana kwa kuwa baadhi ya mashitaka kati ya 20 waliyoshitakiwa hayana dhamana kwa mujibu wa sheria

Kesi hiyo iliahirishwa na itarudi tena Oktoba 30 mwaka huu kwa kutajwa
Previous
Next Post »