Moto uliozuka katika harusi moja nchini Saudia umewauawa watu ishirini na tano na kuwajeruhi wengine thelathini.
Maafisa wa serikali wanasema waathiriwa wote walikuwa wanawake na watoto.
Moto huo uliozuka katika eneo la Abqaiq, unaaminika kuwaka katika transfoma ya umeme iliyoanguka baada ya kugongwa na risasi zilizofyatuliwa wakati wa sherehe hizo.
Bustani ambako sherehe hizo zilifanyika ilikuwa na mlango mmoja wa kutokea nje na waathiriwa wengi wanaripotiwa kuwa wamepigwa na umeme katika harakati za kujaribu kujiokoa.
EmoticonEmoticon