WATANO WAFA MBEYA AKIWEMO MAMA NA NA WATOTO WAKE WAWILI
WATU watano wamefariki dunia mkoani Mbeya katika
matukio matatu tofauti likiwemo la familia ya mama na watoto wake wawili
waliofariki kufuatia ajali ya moto ulioteketeza nyumba yao wakiwa
wamelala.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoani
Mbeya mrakibu mwandamizi Barakiel Masaki, tukio hilo
lilitokea Agosti 16 mwaka huu majira ya saa 4:55
usiku.
Alisema wanafamilia hao wakiwa wamelala nyumba yao
ilianza kuwaka moto na kwamba walipoteza maisha kutokana na kukosa hewa kufuatia
moshi mzito ulioenea ndani ya nyumba.
Amewataja wanafamilia hao
waliokufa ni mama mzazi Upendo Paul(24) na watoto wake ambao ni
Tecra Paul (4) na Aman Paul wote wakazi wa Ilemi darajani jijini
Mbeya.
Masaki alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo mpaka sasa
bado hakijajulikana na miili ya maremu hao imehifadhiwa katika hospitali ya
rufaa mkoani hapa.
Aidha ametoa wito kwa
wananchi kuchukua tahadhari kutokana na majanga ya moto
yanayotokea mkoani hapa.
Wakati huo huo mkazi wa majengo Mkwajuni
wilayani Chunya Sprian Majiyashamba(58) anashikiliwa na
jeshi la polisi baada ya kuumua mke wake kwa kumchoma kisu
kutokana ugomvi wa kifamilia.
Kaimu kamanda Masaki amesema
marehemu alifahamika kwa jina la Secilia
Dotabarabara(64) ambaye alichomwa kisu na mume wake kwenye titi la kushoto na
kusababisha kifo chake papo hapo.
Masaki amesema kuwatukio hilo
lilitokea Agosti 16 mwaka 2012 majira ya saa 4:00 katika kijiji cha
majengo wilayani chunya na kutaja chanzo cha kifo hicho kuwa ni
ugomvi wa kifamilia.
Katika tukio lingine mwanamke mmoja mkazi wa kijiji
cha nyakazobe wilayani Mbarali amemuua mume wake kwa
kumpiga na kitu kitu kizito kichwani kutokana kutokana na na
ugomvi wa kifamilia.
Akielezea tukio hili Masaki
amesema limetokea Agosti 16 mwaka huu majira ya saa 3:00 usiku kijijini
hapo,na kwamba Christina Msiyunga(24) alimuua mume wake Geoge Lova(26) kwa
kumpiga na kitu kizito kichwani na kusababisha kifo chake papo
hapo.
Amesema mtuhumiwa wa
tukio hilio amekamtwa na atafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi
kukamilika,aidha aliwaomba wananchi kutatua migogoro kwa amani ili
kuepukana na vifo visivyo vya lazima.
EmoticonEmoticon