Enzi za Furaha, Mandla Mandela na mkewe |
|||||||||||
Mandla
Mandela ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela, amemfukuza mke wake mrembo wa Ufaransa, Anais Grimaud baada ya
kugundulika kuwa mtoto aliyejifungua mwezi septemba mwaka jana si wa
kwake. Vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa mtoto huyo hakuwa mtoto wa Mandla hivyo kupelekea familia ya Mandela kuamua mwanamke huyo arudishwe kwao kwa kuitia aibu familia hiyo. Kali ya yote ni kwamba Anais anadaiwa kupewa na mimba hiyo na kaka yake Mandla kufuatia uhusiano wao wa siri wa kimapenzi wakati Mandla alipokuwa safarini. "Familia ya Mandela imeamua kumrudisha Nkosikazi Nobubele Mandela (nee Anais Grimaud) kwa familia yake baada ta kugundulika kuwa alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa kaka zangu". "Nathibitisha kuwa uhusiano huo nje ya ndoa ulipelekea kuzaliwa kwa mtoto Qheya mwezi septemba mwaka jana" ilisema sehemu ya taarifa ya mjukuu huyo wa Mandela. Baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyo mwaka jana, Mandla na Mkewe walimkabidhi mzee Mandela mtoto huyo na Mzee Mandela alimpa jina mtoto huyo katika sherehe iliyofanyika septemba 16 mwaka jana. Wakati Mandla Mandela akidai kuwa mtoto huyo ni wa mmoja wa kaka zake, Ndaba Mandela ambaye ni mshukiwa mkubwa wa kutembea na mke wa mdogo wake alikanusha kuwa mtoto huyo si wake. | Mandla
Mandela ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson
Mandela, amemfukuza mke wake mrembo wa Ufaransa, Anais Grimaud baada ya
kugundulika kuwa mtoto aliyejifungua mwezi septemba mwaka jana si wa
kwake. Vipimo vya DNA vilithibitisha kuwa mtoto huyo hakuwa mtoto wa Mandla hivyo kupelekea familia ya Mandela kuamua mwanamke huyo arudishwe kwao kwa kuitia aibu familia hiyo. Kali ya yote ni kwamba Anais anadaiwa kupewa na mimba hiyo na kaka yake Mandla kufuatia uhusiano wao wa siri wa kimapenzi wakati Mandla alipokuwa safarini. "Familia ya Mandela imeamua kumrudisha Nkosikazi Nobubele Mandela (nee Anais Grimaud) kwa familia yake baada ta kugundulika kuwa alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa kaka zangu". "Nathibitisha kuwa uhusiano huo nje ya ndoa ulipelekea kuzaliwa kwa mtoto Qheya mwezi septemba mwaka jana" ilisema sehemu ya taarifa ya mjukuu huyo wa Mandela. Baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyo mwaka jana, Mandla na Mkewe walimkabidhi mzee Mandela mtoto huyo na Mzee Mandela alimpa jina mtoto huyo katika sherehe iliyofanyika septemba 16 mwaka jana. Wakati Mandla Mandela akidai kuwa mtoto huyo ni wa mmoja wa kaka zake, Ndaba Mandela ambaye ni mshukiwa mkubwa wa kutembea na mke wa mdogo wake alikanusha kuwa mtoto huyo si wake. |
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon