JUMA NATURE AINGIA NA MALAPA STUDIO ZA EATV JANA



Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Juma kassim kiroboto aka juma nature jana kawaacha watu hoi baada ya kuonekana katika kipindi cha friday night live kinachorushwa na runinga ya EATV.

Mtangazaji wa show hiyo Sam misago alionesha kutofurahishwa na kitendo cha juma nature kutokea kwenye interview akiwa kavaa kandambili aka ndala lakini juma nature hakujali wala nini alionekana kujiamini na kutokujuta kuvaa ndala wakati wa interview.

 Hata hivyo mpenzi wa zamani wa msanii huyo SINTAH alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika kipindi cha friday night live na alimtetea juma nature kwa kusema inawezekana ametoka kufuturu muda si mrefu ndio maana kaja na ndala studio.

 Katika hatua nyingine JUMA NATURE alithibitisha tetesi zilizzozkuwa zimezagaa mtaani kuwa msanii yoyote anaetaka collabo na yeye ni lazima collabo hiyo ifanyike katika studio zake za halisi recorcods.

 Msanii yoyote anaetaka collabo na mimi ni lazima collabo hiyo ifanyike halisi recorcords au bongo records alisema juma nature. juma nature ni miongoni mwa wasanii wanaoongoza kuwa na idadi kubwa ya mashabiki nchini Tanzania na siyo mtu wa majivuno amekuwa akiishi maisha ya kawaida kama wananchi wengine wenye kipato cha chini hii inamtofautisha juma nature na wasanii wengi nchini
Previous
Next Post »