OFISI ZA BENCHMARK PRODUCTION ZATEKETEA KWA MOTO JANA

 

Habari nilizozipata wakati nikisikiliza Amplifaya ya Clouds Fm zinasema kuwa ofisi za Benchmark Production zinazomilikiwa na Madam Ritha Paulsen zimeungua kwa moto jana usiku.  

Kwa mujibu wa habari hizo chanzo cha moto huo ni hitirafu ya umeme kwenye transifoma iliyokuwa karibu na ofisi hizo maeneo ya Mbezi hali iliyoleta kuwaka kwa moto ambapo mali za ofisi hiyo zenye thamani ya zaidi ya Milioni 50 zimeteketea kwa moto huo. 

 Kwenye tukio jingine Madam Ritha ameporwa begi lake dogo la mkononi lililokuwa na kiasi cha pesa takribani Milioni tatu,vitambulisho vyake,kadi za benki pamoja na funguo za gari lake aina ya Benzi vitu ambavyo hadi sasa havijafanikiwa kupatikana na ametoa wito kwa yeyote mwenye kuwa na ufunguo huo wa gari lake anaomba aufikishe Clouds media au kuupeleka kwake mwenyewe.

Previous
Next Post »