Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP),
Mohamed Mpinga (wa pili kushoto), akizungumza na wamiliki wa shule za
udereva (hawapo pichani), wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama cha
Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta), Hoteli ya Dreamers
Buguruni Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus
Sokoni, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla na Katibu wa
chama hicho, Jonas Mhati
Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla (katikati), akimkabidhi risala yao Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP), Mohamed Mpinga. Kulia ni Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (ASP), Deus Sokoni.
Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati (kushoto), akizungumza kwenye mkutano huo.
Katibu wa chama hicho, Jonas Mhati (kushoto), akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mjumbe wa chama hicho, Cosmas Munuo (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
Mjumbe wa chama hicho, Regina Sulle akiuliza swali kwenye mkutano huo. Kushoto ni mjumbe Fatma Somji na kulia ni Santos Akyo.
Mkuu
wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa Polisi (DCP),
Mohamed Mpinga (kushoto), akisisita jambo wakati akijibu maswali ya
wanachama wa chama hicho. Kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Robert Mkolla.
Mjumbe wa mkutano huo, Leonard Mtandika akiuliza swali. Kutoka kulia ni Pascol Mtandika na Ibrahim Nyato.
Mjumbe
wa Mkutano huo kutoka mkoani Dodoma, Robert Mwinje (kulia), akichangia
jambo kwenye mkutano huo.. Kushoto ni mjumbe mwenzake,kutoka mkoani
Mwanza, Mussa Ramadhan.
Mwanasheria
wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi
(ASP), Deus Sokoni (kulia), akifafanua baadhi ya vifungu vya sheria
katika mkutano huo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi, DCP Mohamed Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo ambao ni wanachama wa Chashubuta.
Hapa DCP Mpinga akiagana na wajumbe hao baada ya kufungua mkutano huo.
Na Dotto Mwaibale
JESHI
la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limesema litavifungia vyuo vyote
vinavyotoa mafunzo ya udereva nchini bila ya kuwa na sifa.
Kauli
hiyo ameitoa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Kamishina wa
Polisi (DCP) Mohamed Mpinga wakati akifungua mkutano wa pili wa Chama
cha Shule Binafsi za Udereva Tanzania (Chashubuta) uliofanyika Dar es
Salaam leo.
"Kuanzia
sasa Jeshi la Polisi halitasita kukifungia chuo chochote cha udereva
kitakachokosa sifa kwani kwa kulea shule mbovu tutaendelea kupata ajali
na hivyo kuongeza vifo na majeruhi" alisema Mpinga.
Mpinga
alisema kwa mujibu wa sheria ya shule za udereva sura 163 ya 1965 (R.E
2002) mpaka sasa jeshi la polisi limesajili shule za udereva 260 ambazo
zitategemewa kutoa madereva bora wenye ueledi wa kutosha kutokana na
kuwa chanzo kikubwa cha ajali ni makosa ya kibinadamu ambayo yanafanywa
na madereva.
Alisema
jeshi hilo litafanya msako nchi nzima kuvibaini vyuo ambavyo havisa
sifa na wamiliki wake kuchukuliwa hatua na kuwafikisha kwenye mkono wa
sheria.
Mwenyekiti
wa Chashubuta Taifa, Robert Mkolla wakati akisoma risala yao mbele ya
Mpinga ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo, alisema moja ya
changamoto waliyonayo ni baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri na
usafirishaji kutoona mchango mkubwa unaofanywa na shule za udereva za
watu binafsi wakiamini kuwa vyuo vinavyotoa elimu nzuri ni vile vya
serikali pekee.
Mkolla
alimuomba Kamanda Mpinga uboreshwaji wa mitaala mara kwa mara ili
kwenda na mahitaji ya barabara, vyombo na wakati na shule hizo ziwe
zinashirikishwa katika kutoa michango ya uboreshaji wa mitaala hiyo.
EmoticonEmoticon