Ajali
iliyohusisha Basi la Kampuniya Ndenjela na basi ndogo aina ya Toyota
Hiace, imetokea mapema leo asubuhi katika eneo la St Agrey Uyole, Jijini
Mbeya na kupelekea watu kadhaa kujeruhiwa, huku wengine wakidhaniwa
kupoteza maisha. Chanzo cha ajali hiyo, inaelezwa kwamba ni basi hilo
dogo kuingia barabara kubwa bila ya tahadhali, hali iliyopelekea
kugongwa na Basi hilo la Ndenjela lililokuwa safarini kuelekea Jijini
Dar es salaam.
EmoticonEmoticon