Mkazi
wa kijiji cha Kalovya – Inyonga wilayani Mlele, Ramadhani Ally (20)
amefariki dunia akipatiwa matibabu hospitalini baada kupigwa na
kijana mwenzake.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahri Kidavashari amesema kuwa Ramadhani
alifikwa na umauti baada ya kujeruhiwa na kijana mwenzake Ntema
Kabembenya( 26), mkazi wa kijiji cha Ipwaga.
Kidavashari
amesema tukio hilo lilitokea Januari 22, mwaka huu saa 12:55 jioni
ambapo Ntema alimkuta Ramadhani (marehemu) akimtongoza dada yake
(Ntemwa) mwenye umri wa miaka 12 (jina limehifadhiwa).
“Ntemwa
alikasirishwa na kitendo cha Ramadhani kumtongoza dada yake mwenye umri
wa miaka 12, alimshambulia Ramadhani kwa kumpiga na fimbo na kumjeruhi
vibaya,” alieleza Kamanda Kidavashari.
Inadaiwa
Ramadhani alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Mlele kwa matibabu
lakini alifariki dunia siku iliyofuata akiwa anatibiwa.
Kwa
mujibu wa Kidavashari, mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi ambapo
anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.
EmoticonEmoticon