Watu 14 wauawa, 14 wajeruhiwa kwa risasi mjini California, Marekani

Farhan Khan Shemeji wa mshukiwa aliyehusika na mauaji hayo akizungumza na vyombo vya habari
Farhan Khan Shemeji wa mshukiwa aliyehusika na mauaji hayo akizungumza na vyombo vya habari
Polisi nchini Marekani wamesema takriban watu 14 wameuawa na wengine 14 kujeruhiwa baada ya kupigwa risasi na watu wenye silaha katika mji wa San Bernadino mashariki mwa Los Angeles, California.
Polisi mjini humo inasema tukio hilo limetokea kwenye kituo cha huduma kwa watu wenye ulemavu na inawezekana lilihusisha watu watatu wenye silaha ambao wametoroka kwa gari.
Afisa wa FBI akizungumza na waandishi wa habari na kudai hawajui kuwa hilo ni tukio la kigaidi
Afisa wa FBI akizungumza na waandishi wa habari na kudai hawajui kuwa hilo ni tukio la kigaidi
Watu hao wenye silaha wanasemakana walivalia kijeshi na walitumia silaha za masafa marefu.
Mkuu wa kituo hicho cha watu wenye ulemavu palipoteka mauaji hayo ya kinyama anasema milio ya risasi ilisikika katika jengo lililokodishwa kwa ajili ya hafla iliyoandaliwa na Idara ya Afya.
Watu 14 waliuawa na wengine 14 kujeruhiwa mjiini Los Angeles
Watu 14 waliuawa na wengine 14 kujeruhiwa mjiini Los Angeles
Rais wa Marekani Barack Obama amelaani shambulio hilo na kusema Marekani imekumbwa na tukio la mauaji ya watu wengi ambalo halifanani na jingine lolote duniani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la kijasusi la FBI David Bowdich anasema sababu kubwa ya mauaji hadi haijafahamika.
Watu wa dharura wakijaribu kuwasaidia waathiriwa katika eneo hilo
Watu wa dharura wakijaribu kuwasaidia waathiriwa katika eneo hilo
“Kwa wakati huu ninaelewa moja ya maswali yenu ni kuhusu tukio hili la kigaidi. Ninawaeleza sasa kuwa hatujui kama hili ni tukio la kigaidi kwa hiyo tunaanzia mwanzo kufanya kazi na wenzetu waliopo katika eneo hili.
Hilo ni tukio la 13 la mauaji katika utawala wa Barack Obama
Hilo ni tukio la 13 la mauaji katika utawala wa Barack Obama
Tunadhani inaweza kuwa, pia inaweza isiwe lakini tunafanya kazi bega kwa bega nao kuanzia mwanzo. Kama mambo yatabadilika tupo hapa na hakuna hatua yoyote itakayopotea wakati uchunguzi utakapokuwa unaendelea,” alisema.
Chanzo: BBC Swahili
Previous
Next Post »