Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na watuhumiwa 40 washikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum kwa tuhuma za ukwepaji kulipa kodi pamoja na mtu mmoja ambaye anatafutwa na Jeshi la Polisi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES LTD, ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini.
Kamanda
wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova akionyesha
picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya REGIONAL CARGO SERVICES
LTD,ABDULKADIR S/O KASSIM ABDI, Miaka 38, Mkazi wa Temeke Mikoroshini
ambaye anatuhumiwa kwa kutoa makontena 329 kwenye bandari kavu ya AZAM
(AZAM ICD) bila kulipia kodi anayetafutwa na jeshi hilo pia ni mmoja wa
wakurugenzi wa kampuni za “JAS EXPRESS FREIGHT LTD” na “XL CLEARING AND
FOWARDING Co. LTD” ambazo zote zilitumika kutoa makontena hayo.
Ameonyesha picha ya mtuhumiwa huyo wakati akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam .
Meneja
wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), Diana Masalla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam leo kuhusiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Kukusanya jumla
ya shilingi 10,075,979,462.08 kutoka kwa makampuni 22 ambayo yalihusika
na uondoshwaji wa makontena bandarini kinyume cha sheria na taratibu za
forodha hadi kufikia tarehe 10 Desemba 2015.
Baadhi
ya Waandishi wa habari waliohudhulia katika mkutano na Kamanda wa Kanda
Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Suleiman Kova wakimsikiliza leo
jijini Dar es Salaam.
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es
Salaam linawashikilia watuhumiwa 40 ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula
njama na kuikosesha serikali mapato. Uchunguzi unafanywa kwa pamoja na
maafisa wa Jeshi la Polisi na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo
la kubaini jinsi ambavyo makontena 329 na mengine 2489 yalivyotolewa
bandarini kinyume cha taratibu.
Kati ya hao, watuhumiwa 26 ni watumishi
wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)na watumishi 03 kutoka Bandari kavu
(ICD) YA AZAM wanatuhumiwa kuhusika na upotevu wa makontena 329. Aidha,
watuhumiwa 11 ambao ni watumishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)
kwa kuhusika na upotevu wa makontena 2489.
Uchunguzi unaoendelea pia unahusisha
kupitia kumbukumbu mbalimbali na kadhia za forodha ili kubaini mtindo
uliotumika na kuwabaini wote waliohusika katika mchakato huo. Makontena
329 yaligundulika kukosekana kwenye ICD ya AZAM kuanzia mwezi Julai hadi
Novemba 2015, wakati makontena 2489 yaligundulika kutolewa Bandarini
kuanzia Mwezi Machi mpaka Septemba, Mwaka 2014 kinyume cha taratibu kwa
lengo la kukwepa kodi na ushuru.
Uchunguzi bado unaendelea ili kuwabaini
wote wanaohusika na hatimaye majalada ya kesi yatapelekwa kwa
mwanasheria wa serikali ili watuhumiwa watakaobainika kuhusika na makosa
mbalimbali wafikishwe mahakamani.
Pia kati ya hao makampuni 06 amesema
kuwa yamelipa kodi yote iliyokadiriwa pamoja na adhabu, ambapo makampuni
16 yamelipa sehemu ya kodi iliyokadiriwa pamoja na adhabu.
Aidha, makampuni 26 hayajalipa kodi kiasi cha shilingi 4,789,924,609.69 pamoja na kwamba zoezi la ukadiriaji limefanyika.
hata hivyo amesema kuwa leo ni siku ya
mwisho iliyotolewa na Mheshimiwa Rais kwa wafanyabiashara
waliokwepakulipa kodi ya makontena,
Amewasisitiza wananchi wote watoe
taarifa kuhusu vitendo vya ukwepaji kodi kutumia namba 0784210209. Pia
taarifa za mwenendo wa wafanyakazi wa TRA Wasio waadilifu zitolewe
kupitia simu namba 0689 122515 na ujumbe mfupi 0689 122516.
EmoticonEmoticon