Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya dola za marekani 20,000 kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Neema Shosho kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam jana. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda (kushoto).
|
Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Bihage Edward kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam jana. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda (kushoto).
Dar es Salaam, -Kampuni ya Tigo ikishirikiana na shirika
lisilokuwa la kiserikali la Reach for Change wametoa jumla ya dola 40,000 kwa washindi
wawili wa shindano la ubunifu kwa wajasiriamali wanaotumia teknolojia ya kidijitali.
Kila mshindi amepewa dola 20,000.
Shindano hilo ambalo ni la nne tangu lilipoanzishwa mwaka 2012, lina
lengo la kuwawezesha wajasiriamali wanaobuni miradi ya teknolojia ya kidijitali
inayosaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.
Washindi wa mwaka huu ni Neema Shosho ambaye kwa kupitia kampuni yake
ya Afya Slices, amebuni mfumo wa teknolojia ya kidijitali unaotoa taarifa
kuhusu lishe kwa watoto na Bihage Edward, aliyebuni mradi wa kutunza vifaa vya
elimu kidijitali unaosaidia kutokomeza ajira kwa watoto na kusambaza taarifa
kwa njia ya ujumbe mfupi kwa kutumia simu za mkononi na kutengeneza programu ya
Mp3 mahsusi kwa kutoa uelewa kuhusu ajira kwa watoto kwa jamii nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu
wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev alisema: “ni furaha kubwa kwetu
kuwatangaza washindi wa mwaka huu wa shindano la ubunifu la Tigo Digital
Change-Makers. Kwa muda wa miaka minne sasa shindano hili limewanufaisha zaidi
ya watoto 10,000 nchini na tunaamini kuwa ongezeko la washindi wawili litaleta
mabadiliko zaidi kwa watoto na kusaidia kuifanya Tanzania kuwa mahala pazuri pa
kushi.
Berdiev alifafanua kwamba maisha ya kidijitali yanakuza teknolojia
yenye mawazo ya kuleta mabadiliko endelevu. “Teknolojia ya kidijitali haibadilishi
tu jinsi tunavyofanya biashara ila pia inasaidia kukuza biashara barani Afrika
na vilevile kuleta mapinduzi ya jinsi ya kutatua matatizo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya kijamii kwa
ujumla”, alisema Berdiev.
Huu ni mwaka wanne ambapo Tigo na shirika la Reach for Change
wanazindua washindi wa shindano hili ambapo washindi huchujwa kutoka kwenye
washindani vijana ambao wana mwamko wa kubuni miradi inayotumia ya kiditali ili
kutatua matatizo mbalimbali ya vijana na watoto katika jamii ya Watanzania.
Afisa Mkuu wa Biashara huyo alisifia kazi mbalimbali za washindi
waliotangulia na kuwatia moyo wengine ili waendelee kubadilishana mawazo.
“Tumepata mafanikio makubwa sana katika kuwapa msukumo
wajasiriali-jamii. Kwa sasa tunasasidia waleta mabadiliko saba ambao kati yao,
watano wana miradi inayoshughulika na masuala ya kidijitali”. Kwa mfano, Carolyne
Ekyariisma anafundisha masomo ya awali ya kompyuta ili kuwapa uwezo vijana wa
kike wenye umri kati ya 10 na 18 ujuzi wa awali katika kutumia kompyuta na
amefanikisha kuwapa ujuzi takribani wanafuzi 500 kwa mwaka 2014 pekee.
Mwingine ni Joan Avit ambaye amejikita katika kutoa elimu bora ya awali
ya watoto kwa kuieneza kupitia njia ya michezo ya kidijitali inayojulikana kama
Grapho Game Tanzania inayowasaidia watoto kujifunza kusoma kwa haraka na kwa
makini na ameweza kuwasaidia watoto 900 kwa mwaka 2014 pekee kupitia mchezo
huu. Naye Faraja Nyalandu anayeendesha mradi wa shule, alibuni maarifa ya elimu
kudijitali ili kuwawezesha watoto na vijana kusoma kwa kupitia mtandao wa
kompyuta na huduma za simu ya mkononi. Kwa kutumia nyenzo hizi aliweza kuwaweze
sha zaidi ya watoto 7,300 mwaka 2014.
Vile vile, tunamuwezesha Thadei
Msumanje ambaye amejikita katika kupunguza pengo lililopo kati ya watumiaji wa
tehama mjini na vijijini ambapo ni watoto wachache tu wanao uwezo wa kutumia tehama
mpaka sasa.
Kuna pia Leka Tingitana ambaye ni mtaalamu wa teknolojia; naye kabuni
suluhisho la tatizo katika sekta ya afya ili kuinua mtandao wa wafanyakazi wa
afya ambao wako mstari wa mbele katika kutoa huduma za afya kwa akina mama
wajawazito”.
Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt, ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika hafla hiyo aliahidi kutoa msaada na kuunga mkono juhudi za
shindano hilo kupitia shirika la msaada la Swedish Development Cooperation
Agency (SIDA), na kusema ataungana na Tigo ili kufanikisha shindano la kila
mwaka la ubunifu wa miradi ya kidigitali unaofanywa na wajasiriamali-jamii wa
kitanzania.
“Kwa miaka mingi sasa shirika la maendeleo la SIDA limekuwa mstari wa
mbele kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo hapa Tanzania katika harakati
za kupunguza umasikini uliokithiri miongoni mwa wananchi hasa vijana, watoto na
akina mama”, alisema.
Alisema ya kwamba amefarijika mno kwamba sasa nchi yake itashirikiana
na kampuni ya Tigo ambayo ni taasisi inayojituma kwa dhati katika kutekeleza
malengo yake ya kuisaidia jamii hapa Tanzania kwa kubuni fursa mbalimbali za
maendeleo ili kukusanya mawazo ya kuleta tija katika jamii ya watanzania.
|
EmoticonEmoticon