MADEREVA WAWILI WA GARI LA MAGAZETI YA MWANANCHI WALIOKUWA WAKISAFIRISHA MAGAZETI KWENDA MBEYA WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUPATA AJALI ENEO LA KITONGA

Gari inayosafirisha magazeti ya Mwananchi kuelekea Mbeya na Iringa ikiwa imepata ajali Eneo la Kitonga Iringa leo 

 
 
Watu wawili wamefariki dunia Papo hapo baada ya Gari walilokuwa wakisafiria iliyobeba  Magazeti ya Mwananchi,The Citizen na Mwanaspoti kwenda  mkoani Mbeya kupata ajali Eneo la Kitonga Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa 

Ajali hiyo imetokea   leo alfajiri baada ya dereva wa Gari hilo kujinusuru kugongana USO kwa USO na GARI jingine hivyo kulazimika kuingia nyuma ya lori na kupelekea kifo chao .

Kwa mujibu wa Wakala Afisa mauzo wa magazeti ya Mwananchi Mkoa wa Iringa Alex Kadea ambae alifika Eneo la tukio ameithibitishia mtandao huu wa www . Matukiodaima.co.tz kuwa waliofariki dunia wote wawili walikuwa ni madereva wa Gari hilo .
Previous
Next Post »

EmoticonEmoticon

:)
:(
=(
^_^
:D
=D
=)D
|o|
@@,
;)
:-bd
:-d
:p
:ng