Kamanda
wa Kikosi Usalama barabarani, Mohamed Mpinga (kulia) akimkabidhi zawadi
ya gari aina ya Toyota Sarf, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam,
Jackson Kapongo aliyeshinda kupitia mchezo wa Matumizi bora ya Mitandao
ya Kijamii iliyoendeshwa na Kampuni ya Enhance Auto ya Jijini Dar es
Salaam. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq
Butt.Picha na Father Kidevu Blog.
Mkurugenzi
wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt akionesha stika za kuhamasisha
usalama barabarani ambazo pia zilizinduliwa na Kamanda Mpinga.
Meneja Mauzo Enhance Auto, Ayaka Kashida akionesha shindano jipya ambalo mshindi atajishindia Toyota Noah mpya.
Jackson Kapongo akiwa katika gari yake Toyota Sarf na pembeni yake ni Kamanda Mpinga.

Hii ndio gari jipya Toyota Sarf aliyo jishindia Kapongo. SOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Wageni mbalimbali waalikwa wakifuatilia tukio hilo.
Bahati na sibu ilichezeshwa na wateja kujishindia mipira
Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butta akitoa maelezo ya bahati nasibu ya kushinda mipira.
**************
Na Father Kidevu
MHITIMU
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jackson Kapongo ameibuka mshindi na
kukabidhiwa gari aina ya Toyota surf lenye thamani ya zaidi ya sh
milioni 24 katika shindano lililochezeshwa na kampuni ya kuuza magari ya
Enhance Auto.
Kapongo
alikabidhiwa gari lake hilo na Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani,
Mohamed Mpinga baada ya kushinda katika shindano lililoendeshwa na
Enhance Auto likiwataka washiriki kuonesha ni namna gani wanaweza
kutumia mitandao ya kijamii na kujiletea manufaa.
Akizungumza
kampuni hiyo, Mpinga alisema imekuwa ikichezesha shindano hilo kila
mwaka na kushirikisha nchi mbalimbali Afrika ambapo kwa mwaka jana
mshindi alipatikana kutoka Zambia lakini kwa mwaka huu ameshinda
mtanzania hivyo ni jambo la kujivunia.
Alisema
mbali na kutoa zawadi lakini kampuni hizo za magari zinajukumu kubwa la
kutoa mchango kwa usalama barabarani kwa kutoa elimu sambamba na kuuza
magari yenye viwango vinavyokubalika ili kuepusha ajali zisizo za
lazima.
"Natoa
wito kwa kampuni zingine kuwekeza katika usalama barabarani na
wasifikirie tu kuuza magari bali wahakikishe magari yanakuwa salama na
wanaoendesha wanakuwa salama... tuagize magari yenye viwango mana ajali
nyingi pia zinasababishwa na ubovu wa magari" alisema.
Mapema
Mkurugenzi wa Enhance Auto, Aatif Farooq Butt alisema shindano hilo
mshiriki anatakiwa kushiriki kwa kuchagua mitandao yao ya kijamii kwa
wingi zaidi na lilishirikisha nchi ambazo wanafanya nao biashara ikiwemo
Botswana, Burundi, Jamhuri ya Kongo, Malawi, Msumbiji, Sudan ya Kusini,
Uganda, Zambia, Zimbabwe na Tanzania.
Hata
hivyo alisema kwa kutambua umuhimu wa usalama barabarani kwa
kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha Usalama Barabarani
wameanzisha kampeni ya 'Endesha kwa Usalama' ambapo pia walikabidhi
stika za magari lengo likiwa ni kujenga uhusiano na wateja wao.
Akizungumza
zawadi hiyo, Kapongo aliishukuru kampuni hiyo na kuwataka vijana
kutumia mitandao ya kijamii kwa faida na si kwa kujifunza mambo ambayo
huharibu maadili ya jamii.
EmoticonEmoticon