Dec 10 Rais wa awamu ya tano Dr.John
Pombe Magufuli aliteuwa rasmi baraza la mawaziri, miongoni waliotajwa ni
mbunge wa Ilemela Angelina Mabula ambaye aliteuliwa katika nafasi ya
naibu waziri wa Ardhi.
’Kwanza
namshukuru Mungu…pili namshukuru Rais wa awamo ya tano kunichagua katika
nafasi ya unaibu kwa wana ilemela niseme tu kwamba nawashukuru tu wao
kwasababu wasingenipa nafasi ya ubunge nisingefika hapa nilipo kwahiyo
ningependa kuwaambia kwamba tupo bega kwa bega’ – Angelina
‘Naomba
nikuhakikishia kwamba mimi sio kati ya wale wanaojisahahu kwasababu
dhamana hii niliyopewa ya unaibu waziri ina mikono ya wana ilemela
kwahiyo niseme kwamba nitakuwa pamoja maana unapokuwa waziri au naibu
waziri kuna vipindi ambavyo vipo unatakiwa kuwa jimboni…sikutarajia
nafasi ya kuwa naibu waziri ila kwasababu Mh Rais kuniaminia ndio maana
akanipatia hiyo nafasi’ – Angelina Mabula
EmoticonEmoticon