Katibu Msaidizi wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga(Tanga Press Club) Dege Masoli(L) akipokea Kadi ya 4GLTE toka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu za Mikononi za Tigo Kanda ya Pwani,Goodluck Charles wakati wa uzinduzi wa upatikanaji wa teknologia ya 4GLTE jijini Tanga leo. Tanga, Novemba 25 2015. Wateja wa Tigo waishio Tanga sasa wanaweza kupata mtandao wa intaneti wenye kasi kubwa zaidi kufuatia upanuzi wa upatikanaji wa huduma ya 4G LTE hadi kufikia jiji hilo lilopo kaskazini mwa Tanzania Teknolojia ya 4G LTE ina kasi mara tano zaidi kuliko teknolojia ya 3G inayopatikana nchini kwa sasa.
‘’Upanuzi huu umetokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana
katika majaribio ya awali ya utoaji huduma ya 4G jijini Dar es
Salaam kuanzia mapema mwaka huu’’, amesema Mkurugenzi wa kanda ya Pwani,
Goodluck Charles.
Akizungumza leo na waandishi wa
habari jijini Tanga, Charles amesema: "ni kielelezo cha jinsi ambavyo Tigo
imedhamiria kufanikisha kuleta mabadiliko ya dijitali katika maisha
ya watanzania na pia kuwa katika msitari wa mbele wa kutumia teknolojia ya
kisasa na kibunifu nchini Tanzania."
Mtandao wa 4G LTE una kasi kubwa zaidi katika kuperuzi
na kupakua kwa rahisi kutoka kwenye mtandao wa
intaneti na pia katika kufanya mawasiliano kwa njia ya Skype. Huduma
hii pia inaharakisha urushwaji wa picha za video na
ubora hali ya juu na kufanya mikutano kwa njia ya mtandao.
“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu waishio Tanga
kwamba sasa wanaweza kufurahia huduma bora zaidi za mawasiliano kutoka Tigo na
Intaneti yenye kasi zaidi,” Charles amesema. Tanga ni moja wapo ya miji mikubwa
Tanzania, na pia inajivunia bandari ndani ya Afrika Mashariki na kwa sababu ya
bahari ya Hindi ni kivutio cha utalii nchini.
Wateja wote wa Tigo 4G LTE
watanufaika na promosheni; kila atakapo ongeza salió la shilingi elfu moja au zaidi, atapata mb 500 bure kama
bonasí.
Ametaja miji mingine katika mikoa sita ambapo 4G itaanza
kupatikana hivi karibuni kuwa ni Tanga, Dodoma, Morogoro, Moshi, Mwanza na
Arusha, “jambo ambalo linaifanya Tigo kuwa na mtandao mkubwa wa 4G
nchini Tanzania.” Lengo kuu ni kufikisha huduma ya 4G katika kila kona za
nchi ifikapo mwaka ujao, Charles ameongeza kusema.
Imeandaliwa na :http://bongodailyupdates.blogspot.com/
|
KONA YA JAMII
TIGO TANZANIA
Wakazi wa Tanga waanza kufaidi Intaneti ya kasi zaidi ya 4G LTE toka Tigo
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon