MATOKEO YA UBUNGE MAJIMBO YA MKOANI MBEYA HAYA HAPA



Jimbo la Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi(Chadema) ameshinda kwa kupata kura 97,675,Mwalyego Shitambala(CCM)46,894,Amin Ashery(ACT)696,Mary Komba(Chausta)202 na Oswald Mwanyalu(Makini)96.



Jimbo la Mbeya vijijini Oran Njeza(CCM) ameshinda kwa kupata kura 56,301,Zera Abraham(Chadema)52,298,Barick Mwanyaru(makini)421.



Jimbo la Kyela Dk.Harison Mwakyembe(CCM) ameshinda kwa kupata kura 44,269 na Abraham Mwanyamaki(Chadema) kura 38,375,Samwel Andrea(ACT) kura 275 na Zamoyoni Peter(DP) kura 201.



Jimbo la Rungwe Henry Saul(CCM) ameshinda kwa kupata kura 44,745 akifuatiwa na John Mwambigija(Chadema) kura 43,613,Farank George(ACT) 1,042,Nicodemas Ngwala(DP)620,Fredy Mwandembe(UDP)419.



Jimbo Ileje,Janeth Mbene(CCM) ameshinda akipata kura 27,582,Emmanuel Mbuba(Nccr) 14,578,Nuru Magiji(ACT) 654.



Jimbo la Mbarali,Pirmohamed Mulla(CCM) ameshinda kwa kupata kura 45,352,Liberatus Mwang’ombe(Chadema) 36,603,Modest Kirufi(ACT) 20,606.



Busokelo Atupele Mwakibete(CCM) ameshinda kwa kupata kura 20,206,Boniface Mwabukusi(Chadema) 12,807,Gwandumi Mwakatobe(ACT) 261 na Ambakisye Mwakifwange(TLP) kura 204.



Jimbo la Mbozi Paschal Haonga(Chadema) ameshinda akipata kura 36,362,Godfray Zambi(CCM) 34,586,Julius Mwanitega(ACT) 732.



Jimbo la Vwawa Japhet Hasunga(CCM) ameshinda kwa kupata kura 36,705,Fanuel Mkisi(Chadema)35,400 na Rose Mwashambwa(ACT) 502.



Jimbo la Tunduma Frank Mwakajoka(Chadema) ameshinda kwa kupata kura 32,442,Frank Sichalwe(CCM) 17,220,Reddy Makuba(ACT) 319 na James Mwakalonge(TLP) 85.



Jimbo la Momba,David Silinde(Chadema) ameshinda kwa kura 26,468 akimshinda mbunge wa Zamani wa Mbozi Magharibi Dk.Lucas Siyame(CCM) aliyepata kura 26,260 na Weston Simwelu(ACT)1,156.
  

Jimbo la Lupa,Victor Mwambalaswa(CCM) ameshinda kwa kupata kura 32,413 akifuatiwa na Njeru Kasaka(Chadema) kura 22,147 na Muhamed Hussen(ACT) amepata kura 3,907.

Jimbo la Songwe aliyewahi kuwa naibu waziri wa Elimu Filipo Mulugo(CCM) ameshinda kwa kupata kura 29,814 akimshinda mpinzani wake Mpoki Mwakisu(Chadema) aliyepata kura 16,165 na Maiko Nyilawila(ACT) akapata kura 437.


Previous
Next Post »