CHOPA ILIYOPATAAJALI NA KUUWA WATU 4 AKIWEPO FILIKUNJOMBE ILIKUWA YA KALONZO MUSYOKA



 Helokopta aina ya Eurocopter AS 350B3  yenye namba za usajili 5Y-DKK. Ilikuwa na uwezo wa kubeba tani 1.
HELKOPTA iliyoanguka na kusababisha vifo vya watu wanne akiwepo Mgombea Ubunge wa jimbo la Ludewa kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na rubani wake, William Silaa ilikuwa mali ya Makamu wa Rais wa zamani wa Kenya, Kalonzo Musyoka.

Kwa Mujibu wa mtandao  wa The Star wa Kenya, Helkopta hiyo AS 350B3 Eurocopter yenye namba za usajili 5Y-DKK na iliyokuwa na namba ya uzalishaji 7027 na ilikuwa imekodiwa na mgombea huyo wa CCM kwaajili ya kampeni zake jimboni Ludewa.

Mbali na Filikunjombe pia watu wengine wa tatu waliotambulika kuwa ni Rubani wa Helkopta hiyo, Capt. William Silaa, Kasablanka Haule na Egid Mkwela walifariki katika ajali hiyo iliyotokea alhamisi jioni wakati ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Njombe na kuanguka katika Msitu wa akiba wa  Selous Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro.

Helkopta hiyo ilikuwa na uwezo wa kubeba mzigo  usiozidi tani moja na ikiruka urefu wa futi 20,000 kutoka ardhini.

Wachunguzi wa ajali za ndege nchini Tanzania, wamechukua baadhi ya vitu kutoka katika mabaki ya Chopa hiyo iliyoteketea kabisa kwaajili uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Helkopta hiyo ni moja ya Helkopta nyingi zilizosajiliwa nchini Kenya, ambazo zimekudiwa na wagombea mbalimbali wa Urais na Ubunge kwaajili ya kampeni za uchaguzi zinazoendelea.

Kalonzo alinunua helkopta hiyo ya kisasa kwaajili ya kampeni za uchaguzi Mkuu wa 2013 na imekuwa ikikodiwa ndani na nje ya Kenya kwa shughuli mbalimbali.

Kwa mujibu wa mtandao wa www.aircraftcompare.com Helkopta mpya AS350 B3 ina gharimu Shilingi bilioni 4.250 (dola Milioni 1.95) bila gharama za kuinganisha.

Kenya ina ndege binafsi takriban 400 zilizosajiliwa nchini humo ambazo zinamilikiwa na watu binafsi wakiwamo, wakulima wakubwa, wafanyabisahara na wanasiasa mashuhuri.
Previous
Next Post »