Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Ahmed Msangi akionyesha Pembe za Faru kwa Waandishi wa Habari |
Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Kamanda |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Ahmed Msangi akiangalia sehemu ambayo walikuwa wameficha Pembe hizo za Falu.(Picha na David Nyembe wa Fahari News) |
Mwonekano wa Sehemu walipokuwa wameficha Pembe hizo za Falu kwenye Gari. |
POLISI
Mkoani Mbeya, inawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kupatikana na nyara za
serikali ambazo ni pembe za mnyama Faru
kilo tano pamoja na vipande vinne vya
mawe vinavyodhaniwa ni madini yenye
uzito wa kilo moja.
Pembe
hizo, zinadaiwa zinathamani ya zaidi ya milioni 80 wakati thamani ya mawe hayo
yanayodhaniwa kuwa ni ya madini haijajulikana wala ni aina gani ya madini.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya,
Ahmed Msangi, alisema watuhumiwa hao walikamatwa jana majira ya saa nane za
mchana katika mpaka wa Kasumulu unaotenganisha nchi mbili ya Tanzania na
Malawi.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Arquemides Joao Mahanjane akiwa na paspoti namba
13AF5838 na Henriques Benditor Assuba akiwa na pasipoti yenye namba AF24132 wote wakazi wa Maputo nchini
Mozambique.
Akielezea
tukio hilo, Kamanda Msangi alisema kuwa watuhumiwa hao wakiwa kwenye gari namba
za usajili ABL 860 MCaina ya Toyota Hilux Vigo Double Cabin, wakiwa katika harakati
za kuhakiki pasipoti, baahi ya maofisa
wa polisi na idara nyingine waliwatilia shaka na hivyo kufanya upekuzi.
Alisema,
katika upekuzi huo walifanikiwa kukuta nyara hizo mbili za pembe za Faru zenye
thamani ya shilingi milioni 82, 692,000 na vipande vine vya mawe yanayodhaniwa
ni madini ambayo bado hayajajulikana aina yake.
Aidha,
watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Kyela mbele ya hakimu
mfawidhi Roda Martini na kusomewa mashitaka na kupatikana na hatia hi yo
kufungwa jela miaka nane kwa kosa la kupatikana na nyara za serikali kinyume
cha sheria.
EmoticonEmoticon