Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi wa Watoto wenye Ulemavu wa Mtindio wa
Ubongo, Akili na Viungo Tanzania (Chawaumavita), Hillar Said (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Watu, Watoto wenye mtindio wa
ubongo yatakayofanyika, Oktoba 7, 2015 viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa chama hicho, Mwanahamisi Hussein.
Katibu wa chama hicho, Mwanahamisi Hussein (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Wazazi wa Watoto Wenye
Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo (Chawaumavita) kimewataka wakina
baba kuacha tabia ya uoga ya kukimbia majukumu pindi wanapopata watoto wenye
ulemavu.
Katika hatua nyingine chama hicho
kimewaomba wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa kuzungumzia namna gani
watasaidia walemavu katika mikutano yao.
Akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Watu na Watoto
Wenye Mtindio wa Ubongo ambayo huazimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba 7. Makamu
Mwenyekiti wa chama hicho, Hilal Saidi, alisema watoto wenye matatizo hayo
wanapaswa kusaidia badala ya kuwatenga.
Alisema kuwa katika tafiti
walizofanya wamegundua kuwa wanaume wengi ni waoga wa majukumu pindi wanapopata
watoto wenye ulemavu hadi kupelekea kukimbia famia zao.
"Wanaume wengi waoga wa
majukumu hasa anapozaliwa mtoto mwenye ulemavu, wanaona kuwa ni mkosi mkubwa na
kuanza kupata msukumo katika familia yake kuachana na mkewe hivyo anateleleza
familia huku mwanamke akibaki peke yake" alisema Said
Hata hivyo alisema ulemavu
umegawanyika katika makundi matatu ambayo ni ni ulemavu wa akili,mtindio
wa ubongo na viungo.
Alisema watoto wenye ulemavu wa
viongo na mtindio wa ubongo wanaweza kupatiwa matibabu hali yao ikawa sawa
kushiriki katika katika elimu na kufikia malengo yao.
Hivyo aliwataka wakina baba na
familia kwa ujumla kutowafungia ndani watu wenye ulemavu na badala yake
kuwapeleka katika vituo vya afya kwaajili ya matibabu na miili yao ikatengemaa.
EmoticonEmoticon