Mgombea
mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la
Kilindi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga. Miongoni mwa
ahadi aliyoitoa kwa wanaKilindi ni kulishughulikia suala la upatikanaji
wa huduma za maji safi na salama pamoja na ujenzi wa barabara ya
kuingia na kutoka katika Wilaya hiyo.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Kijiji cha Kwediboma wakiwa wamesimamisha msafara wa mgombea mwenza
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan
kuwasikiliza kilio chao alipokuwa akisafiri kuelekea Wilaya ya Kiteto.
Baadhi ya ahadi aliyoitoa Bi. Samia ni pamoja na upimaji wa ardhi ya
vijiji na wilaya ili kumaliza migogoro ya ardhi kwa wafugaji na
wakulima.
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga akizungumza na wanaCCM na wananchi
katika mkutano mdogo wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais,
Bi. Samia Suluhu Hassan uliofanyika Kilindi, Tanga.
Kutoka
kulia ni mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni Muhita akiserebuka
na baadhi ya viongozi na makada wa CCM walioongozana kwenye kampeni za
mgombea mwenza Wilaya ya Kilindi.
Mgombea
mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu
Hassan (kulia) akimtambulisha mgombea ubunge wa Jimbo la Kilindi, Mboni
Muhita kwa wanachama wa CCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Kilindi
kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni Mkoa wa Tanga.
EmoticonEmoticon