NITAFUMUA MIKATABA YA GESI- Mgombea Urais kupitia CHADEMA

Mgombea Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa, amesema ataunda kamati maalumu ya kupitia upya mikataba yote ya gesi ikiwa atachaguliwa kuingia madarakani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu. Lowassa alisema licha ya rasilimali ya gesi ambayo iligunduliwa katika mikoa ya Kusini mwa nchi kuwa na manufaa makubwa kwa Taifa, mikataba iliyoingiwa haina masilahi kwa nchi na watu wake na kwamba inahitaji kupitiwa upya na kufanyiwa marekebisho stahiki.
Previous
Next Post »