Mkurugenzi
wa Idara ya Wakimbizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Harrison Mseke (kushoto) akizungumza na watumishi wa mashirika
mbalimbali yaliyoko katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko
wilayani Kasulu mkoani Kigoma (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia)
aliyetembelea kambi hiyo jana.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia),
akizungumza na watumishi mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa ziara
yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko wilayani
Kasulu mkoani Kigoma. Kambi hiyo inahifadhi wakimbizi kutoka nchi za
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
Daktari
wa Hospitali ya Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu, Florence
Mshana(aliyeshika karatasi), akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil(kushoto), alipotembelea
hospitali hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea kambi ya wakimbizi ya
Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Kambi hiyo inahifadhi
wakimbizi kutoka nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na
Burundi.
Mkuu
wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR)
Kasulu, Amah Assiama-Hillgartner( kushoto), akitoa maelezo kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil(katikati),
aliyetembelea hospitali hospitali hiyo wakati wa ziara yake katika
kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (katikati),
akiongozana na Mkuu wa Kambi ya Nyarugusu (B), Fredrick Nisajile
(kulia) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi
(UNHCR) Ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner (kushoto) wakati wa
ziara ya Katibu Mkuu kambini hapo jana. Kambi ya Nyarugusu iliyoko
wilayani Kasulu mkoani Kigoma inahifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Burundi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwaki l(katikati),
akiongozana na Mkuu wa Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu (B), Fredrick
Nisajile (kulia) na Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia
wakimbizi (UNHCR) ofisi ya Kasulu, Amah Assiama –Hillgartner (kushoto)
wakati wa ziara ya Katibu Mkuu katika makazi ya wakimbizi yaliyopo
Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil,
akimsikiliza mmoja wa maofisa wa Shirika la Chakula Duniani (WFP)
alipotembelea ndani ya mahema wanakoishi wakimbizi katika kambi ya
Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.(PICHA ZOTE NA KITENGO
CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
EmoticonEmoticon