Bondia Davey Browne ambaye ni raia
wa Australia amepoteza maisha siku nne baada ya kupoteza fahamu kufuatia
kipigo cha ‘knock out’ katika pambano la ngumi huko Sidney.
Mwanamasumbwi huyo mwenye miaka 28
alidondoka chini baada ya kupigwa na mpinzani wake Carlo Magali wa
Ufilipino katika raundi ya 12 katika uzani wa super-featherweight ijumaa
iliyopita.
Baada ya kupoteza fahamu alipelekwa hospitali katika chumba cha wagonjwa mahututi hadi mauti ilipomkuta.
EmoticonEmoticon