TAARIFA
YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” LEO TAREHE 04.08.2015.
- WATU WANNE WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUAWA KATIKA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI NA POLISI WILAYA YA MOMBA.
- MAJENGO MAWILI YA SHULE YA SEKONDARI YAUNGUA MOTO WILAYA YA CHUNYA.
- JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI WILAYA YA KYELA.
- JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA WAWILI WAKIWA NA MADINI YADHANIWAYO NI BANDIA WILAYA YA MBEYA.
TUKIO LA KWANZA:
WATU
WANNE WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUAWA KATIKA MAPAMBANO YA KURUSHIANA
RISASI NA POLISI WILAYA YA MOMBA.
KATIKA TUKIO HILO WATU WANNE WANAUME WASIOFAHAMIKA WANAOSADIKIWA
KUWA NI MAJAMBAZI WALIUAWA KATIKA MAJIBIZANO YA KURUSHIANA RISASI NA ASKARI
POLISI.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 03.08.2015 MAJIRA YA SAA 09.00HRS ENEO LA SOGEA,
KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA. AWALI WATU HAO WALIVAMIA DUKANI KWA THADEO SANGA [50], MFANYABIASHARA NA
WAKALA WA KUUZA/KUSAMBAZA BIA ZA TBL, MKAZI WA MAJENGO TUNDUMA.
KATIKA TUKIO HILO MAJAMBAZI HAO [AMBAO KWA SASA NI MAREHEMU] MARA BAADA
YA KUVAMIA ENEO HILO WAKIWA NA SILAHA /BUNDUKI MBILI AINA YA SMG NA STEERING GUN WALIWAWEKA CHINI YA
ULINZI WATUMISHI WA MHANGA PAMOJA NA YEYE MWENYEWE KISHA KUPORA KUTOKA DUKANI
HUMO PESA TSHS 200,000/=, BASTOLA MOJA
NAMBA B-15859 NA GARI T.215 BLZ AINA YA SUZUKI V6 MALI ZA MHANGA NA
KUONDOKA HUKU WAKIFYATUA RISASI HEWANI KUELEKEA BABARBARA YA MBEYA.
HATA HIVYO MAJAMBAZI HAO
WALIPOFIKA ENEO LA CHAPWA WALIPATA AJALI NA GARI HILO HIVYO KUAMUA KULIACHA
GARI NA KUKIMBILIA PORINI. KWA KUWA
TAARIFA ZA TUKIO ZILIKUWA ZIMEFIKISHWA KITUO CHA POLISI TUNDUMA ASKARI POLISI
WALIFIKA MARA MOJA ENEO LA TUKIO NA KUANZA KUWAFUKUZA WATUHUMIWA AMBAO
WALIINGIA MSITUNI KATIKA MAKORONGO MAKUBWA YALIYOPO ENEO HILO NA KUFYATUALIA
RISASI ASKARI POLISI AMBAO NAO WALIJIBU.
KATIKA HARAKATI ZA KURUSHIANA
RISASI ASKARI POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WA ENEO HILO MAJAMBAZI HAO
WALIPIGWA RISASI KUFARIKI DUNIA KUTOKANA NA MAJERAHA YA RISASI KATIKA HARAKATI
HIZO SILAHA MBILI SMG NAMBA 78421
IKIWA NA RISASI 1 NA STEERING MOJA NAMBA KR 13079 IKIWA NA RISASI 5. MAJAMBAZI HAO WALIPOPEKULIWA
BAADA YA KUUAWA MMOJAWAPO ALIKUTWA NA TIKETI YA BASI LA POWER TOOLS LOGISTIC LTD YENYE NAMBA
111683 ILIYOTOLEWA KWA BW MSONDA TAREHE 02.08.2015 IKIONYESHA ALISAFIRI
KUTOKA LUSAKA – ZAMBIA KUJA NAKONDE, MAJAMBAZI WENGINE WALIKUTWA NA SIMU MBILI AINA
YA TECNO NA MTN.
HATA HIVYO KATIKA HARAKATI ZA
KUWAKAMATA /KUKABILIANA NA MAJAMBAZI HAO RAIA WEMA WAWILI WALIOKUWA WANASHIRIKIANA
NA POLISI BEGA BEGA WALIJERUHIWA AMBAO NI 1.
ABBAS SIWALE [22], MKAZI WA CHAPWA ALIYEJERUHIWA KWA KUPIGWA RISASI PAJA
MGUU WA KULIA NA ALIMTAMBUA MOJAWAPO WA MAJAMBAZI HAO KUWA NDIYE ALIYEMJERUHI
NA 2.
ELIAS FONGO [28], MKAZI WA CHAPWA
ALIYEJERUHIWA KICHWANI KWA KUPIGWA KITU BUTU KINACHOSADIKIWA NI JIWE AMBACHO
ANADAI KUPIGWA NA MMOJAWAPO WA MAJAMBAZI HAO.
MPAKA SASA GARI ILIYOPORWA NA
MAJAMBAZI IMEOKOLEWA HATA HIVYO SILAHA
/BASTOLA NAMBA B- 15859 MALI YA BW
THADEO SANGA BADO KUPATIKANA. UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA KUWA MAJAMBAZI
HAO AMBAO MIILI YAO IMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA KUSUBIRI UCHUNGUZI WA
KITABIBU NA UTAMBUZI WANATOKEA NCHI JIRANI YA ZAMBIA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA
KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WASIOWAFAHAMU ILI HATUA ZA
HARAKA ZA KIUCHUNGUZI DHIDI YAO
ZICHUKULIWE. AIDHA ANAWASA WANANCHI HUSUSANI VIJANA KUJITAFUTIA KIPATO KWA NJIA
HALALI KWANI CHANGAMOTO ZA KIMAISHA/MAENDELEO HAZIPATIKANA KWA NJIA YA
MKATO/HARAMU KWA KUTAKA UTAJIRI WA HARAKA. PIA ANATOA RAI KWA YEYEOTE MWENYE
TAARIFA JUU YA SILAHA/BASTOLA HIYO AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA
HARAKA ZIWEZE KUCHUKULIWA.
TUKIO
LA PILI.
MAJENGO
MAWILI YA SHULE YA SEKONDARI YAUNGUA
MOTO WILAYA YA CHUNYA.
KATIKA TUKIO HILO MAJENGO MAWILI
YA SHULE YA SEKONDARI IITWAYO MAWENI YALIUNGUA MOTO, AMBAPO MAJENGO HAYO NI
GHALA LA CHAKULA NA OFISI YA TAALUMA.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 04.08.2015 MAJIRA YA SAA 00:30HRS
KATIKA KIJIJI CHA MAWENI, KATA YA MKWAJUNI TARAFA YA KWIMBA AMBAPO MOTO HUO
ULIZUKA NA KUUNGUZA VYAKULA VYOTE KATIKA STOO HIYO YA SHULE PAMOJA NA BAADHI YA
SAMANI KATIKA OFISI YA TAALUMA. SHULE HIYO NI MALI YA SERIKALI BWENI NA KUTWA IKIWA MCHANGANYIKO WA WAVULANA NA WASICHANA. THAMANI
HALISI YA UHALIFU WA MALI ILIYOTEKETEA BADO KUFAHAMIKA. UCHUNGUZI WA AWALI
UNAONYESHA CHANZO CHA MOTO HUO NI HUJUMA ZA BAADHI YA WANAFUNZI WALIOFUKUZWA
SHULENI HAPO KUTOKANA NA MATATIZO YA UTOVU WA NIDHAMU. MOTO HUO ULIZIMWA KWA
USHIRIKIANA KATI YA WALINZI WA SHULE,WAALIMU NA WANAFUNZI. HAKUNA MADHARA YA
KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA
MAKINI NA KUCHUKUA TAHADHARI KUHUSIANA NA MAJANGA YA MOTO.
TAARIFA YA MISAKO :
JESHI
LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA
KUINGIA NCHINI BILA KIBALI WILAYA YA KYELA.
KATIKA TUKIO HILO WATU WANNE
AMBAO NI 1. NDUNGURESHI NDILEMBO [17] 2. ADAM TAFADHALI [25]
NA 3. SADICK MUHAMED [18] WOTE WAKAZI NA RAI WA NCHINI BURUNDI KWA
KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. KATIKA TUKIO HILO WATUHUMIWA WALIKUTWA
WAMEHIFADHIWA NYUMBANI KWA MTANZANIA
MWANAMKE TUPO SANGA [26]
MKAZI WA KIJIJI CHA LUBELE.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 03.08.2015 MAJIRA YA SAA 22:00HRS HUKO
KATIKA KIJIJI CHA LUBELE – KASUMULU, KATA YA NJISI,TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA
YA KYELA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI WATUHUMIWA WAKABIDHIWE IDARA YA UHAMIAJI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED
Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA
MAKINI NA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWA NI PAMOJA NA WAGENI KUTOKA NJE YA
NCHI.
KATIKA TUKIO LA PILI JESHI LA
POLISI LINAWASHIKILIA WATUHUMIWA WAWILI WAKIWA NA MADINI YADHANIWAYO NI BANDIA
WILAYA YA MBEYA. WATUHUMIWA HAO 1.
GARDEN ANYETIKE [46], MKAZI WA MTAA WA CHEMCHEM NA 2.
MBOKA MWAMBETE [37], MKAZI WA UYOLE WALIKAMATWA WAKIWA NA MADINI
YADHANIWAYO KUWA NI BANDIA YENYE UZITO WA GRAM
20.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 03.08.2015 MAJIRA YA SAA 18:30HRS
HUKO ENEO LA ITEZI, KATA YA ITEZI, TARAFA YA IYUNGA JIJINI MBEYA. UCHUNGUZI
ZAIDI BADO UNAENDELEA.
Imetolewa na:
AHMED .Z. MSANGI – SACP
KAMANDA
WA POLISI [M] MBEYA
EmoticonEmoticon