TANGAZO
KWA UMMA.
MNAMO TAREHE 10/08/2015
OFISI YA MKUU WA POLISI WILAYA YA MBEYA ILIPOKEA BARUA TOKA CHAMA CHA
DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) INAYOHUSU TAARIFA YA MKUTANO WA HADHARA
UTAKAOFANYIKA TAREHE 14/08/2015 KATIKA VIWANJA VYA RUANDA NZOVWE.LENGO LA
MKUTANO HUO NI MGOMBEA WA RAISI KUOMBA WADHAMINI
LEO TAREHE 13/08/2015 JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LILIKUTANA NA
UONGOZI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO AKIWEMO MBUNGE WA MBEYA MJINI NA
BAADHI YA MADIWANI KATIKA ENEO LA USALAMA WA CHAMA HICHO KATIKA OFISI YA
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA NA KUFANYA MAZUNGUMZO KISHA KUFIKIA MAKUBALIANO
KAMA WALIVYOTOA TAARIFA YAO KUWA HAKUTAKUWA NA MAANDAMANO BALI NI MKUTANO. HII
INATOKANA NA;
-
SABABU ZA KIUSALAMA
-
KUTOZUIA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA HIYO
IKIZINGATIWA BARABARA KUU ITAKAYOTUMIKA NI MOJA.
HIVYO BASI KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA ANATOA RAI KWA WANANCHI KUTOFANYA AU KULAZIMISHA
MAANDAMANO YOYOTE YAWE YA MIGUU AU PIKIPIKI.HII IELEWEKE KWAMBA SI MAANDAMANO
BALI NI MKUTANO WA HADHARA UTAKAOFANYIKA KATIKA VIWANJA HIVYO. KINYUME NA HAPO
HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA.
IMETOLEWA NA:
AHMED
Z.MSANGI – KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon