Tanzania inatarajia kuwa wenyeji wa fainali za Afrika za
soka kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019.
Akizungumza leo jijini Dar es salaam Rais wa shirikisho
la soka la Tanzania (Tff) Jamal Emmily Malinzi amethibitisha kuwa Tanzania
watakuwa wenyeji wa fainali hizo .
Amesema Tff kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania
walituma maombi katika shirikisho la soka la Afrika (CAF) kuomba kuwa wenyeji
wa fainali hizo na hatimaye Caf imeridhia Tanzania kuwa wenyeji mashindano
hayo.
Na shirikisho la soka Tanzania (Tff) likiwa katika mikakati ya maandalizi ya fainali hizo, Rais huyo amewataka wadau mbalimbali wa soka nchini yakiwemo mashirika ya watu binafsi , sekta binafs i kujitokeza na kutoa michango ya fedha na vifaa kwa lengo la kufanikisha fainali hizo na hatimaye kuweza kujitangaza kisoka kupitia fainali za afrika kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 17.wa mujibu wa BBC
EmoticonEmoticon