WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.



TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 16.07.2015.

·         WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA.

·         MTOTO WA MIAKA SABA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
 
·         WATU WATANO WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KATIKA MATUKIO TOFAUTI.
 
KATIKA TUKIO LA KWANZA:

WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. IBRAHIM HASSAN (41) MKAZI WA MSWISWI NA 2. MWANAMKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MAMA BONI, MKAZI WA UYOLE WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA GARI AINA YA MITSUBISHI FUSO IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA KUGONGANA NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.478 BSW AINA YA TOYOTA HAICE IKIENDESHWA NA DEREVA MAWAZO FAUSTINE (40) MKAZI WA IGURUSI.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.07.2015 MAJIRA YA SAA 19:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI, KATA NA TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE.

AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WAWILI WALIJERUHIWA AMBAO NI HURUMA BARTON (38) MKAZI WA NONDE NA SOPHIA KAMWELA (67) MKAZI WA NONDE AMBAO WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.

MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA TOYOTA HAICE. DEREVA WA FUSO ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI.



KATIKA TUKIO LA PILI:

MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 07 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MICHAEL ALLY @ KUNDWE MKAZI WA MAHENJE ALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI YENYE NAMBA IT 2046 AINA YA MAZDA IKIENDESHWA NA DEREVA EMANUEL HALISON @ MBWANA (43) MKAZI WA DSM.

AJALI HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 15.07.2015 MAJIRA YA SAA 19:30 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHENJE, KATA YA MAHENJE, TARAFA YA IYULA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU MBEYA/TUNDUMA.

CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMEKAMATWA. UPELELEZI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA, ALAMA NA MICHORO YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
 
TAARIFA ZA MISAKO:

KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ASUMIN ALLY (47) MKAZI WA MADUMBWI WILAYANI CHUNYA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 5.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.07.2015 MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MADUMBWI, KIJIJI NA KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO WA PILI, MTU MMOJA MKAZI WA MADUMBWI WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LUCAS SWEHA (63) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 3.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.07.2015 MAJIRA YA SAA 15:30 JIONI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MADUMBWI, KIJIJI NA KATA YA MAMBA, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.


KATIKA MSAKO WA TATU, MWANAMKE MMOJA MKAZI WA MAPELELE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUDITH MSONGWE (28) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA ANAUZA POMBE YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 2.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 15.07.2015 MAJIRA YA SAA 10:00 ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA MAPELELE-MBALIZI, KATA YA SONGWE, TARAFA YA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.

KATIKA MSAKO WA NNE, MTU MMOJA MKAZI WA BAGAMOYO WILAYANI RUNGWE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BASTER ALEX (27) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI GRAM 30.

MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 15.07.2015 MAJIRA YA SAA 11:24 ASUBUHI HUKO KATIKA MTAA WA BAGAMOYO, KATA NA TARAFA YA TUKUYU, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.

TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI NA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »