VIJANA WALIOSAFIRI KWA BAISKELI KUTOKA MBEYA KWENDA IKULU KUMPONGEZA MHESHIMIWA RAIS KWA UONGOZI WAKE WAFANIKISHA LENGO LAO



Ukiweka malengo au lengo ya kufanya jambo fulani haijalishi kwako itakuchukua muda gani, yatakuwa na ugumu kiasi gani au utakutana na changamoto kiasi gani?
Mwisho wa siku ni lazima kutimiza lengo hilo.
Jiamini Mwenyewe Unaweza; ya kwamba umezaliwa una kipawa au uwezo wako halisi ambao Mungu kaweka ndani yako hivyo amini ya kwamba wewe ni mshindi unaweza hakuna chochote kile mbele yako kitachofanya wewe ushindwe.
Amini Mungu kwa kile unachokifanya ya kwamba Mungu yeye atakibariki na kuwezesha kifanikiwe.
Hakuna kukata tamaa, kukata tamaa ni mwiko katika kufanikisha kile ambacho umekipanga au umekidhamiria kufanya katika kuelekea Mafanikio.
"Penye nia pana njia", siku zote ukiwa na nia ya kufanya jambo fulani ukiwa na nia ya dhati na jambo hilo hata liwe na changamoto kiasi gani? njia ya kulifanikisha jambo hilo itapatikana tu.
Kuthubutu, utayari wa kufanya jambo fulani nalo ni suala muhimu sana ukiwa una lengo fulani, Je upo tayari kufanyia kazi maamuzi mara moja bila kujiuliza mara nyingi sana. Na pia kuona wengine watakuona vipi au watasema nini juu yako watakufikiria vipi juu ya kile unachotaka kufanya?
"Mafanikio ni matamu lakini safari ya mafanikio ni chungu mno" ukitaka mafanikio ni lazima ujue ya kwamba kuna mambo machungu au magumu utakutana nayo katika safari yako ya mafanikio hivyo basi uwe tayari kujitoa kikweli kwa dhati.

"Chochote kile ambacho unacho na una lengo ya kukifanya inawezekana kufanikiwa"Hayo ni maneno ya mmoja wa vijana hao Wiseman Tanzania

Previous
Next Post »