MCHAICHAI NI ZAIDI YA KIUNGO NA HIZI HAPA NDIO FAIDA ZAKE

 
Fahamu juu ya mchaichai au Lemongrass tea
Je! unafahamu kuwa majani ya mchaichai yana faida kubwa kiafya na Mafuta ya mchachai hutumika katika viwanda vinavyotengeneza pafyumu na sabuni??

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa mchaichai una vichocheo muhimu vinavyoweza kupambana na athari kadha wa kadha tumboni, kwenye mkojo na hata kwenye vidonda. Watu wengine huamini kuwa mchaichai unaweza kutibu baadhi ya maradhi kama vile homa ya matumbo, matatizo ya ngozi, madhara yanayotokana na ulaji wa chakula chenye uchafu na pia hutibu maradhi ya kichwa na hata misuli.
Mchaichai pia unatajwa kuwa kinywaji kinachoweza kupunguza joto. Chai ya mchaichai inasaidia kupunguza joto kwa mgonjwa wa homa. Faida nyingine za mchaichai kiafya ni pamoja na:
- Kinga dhidi ya saratani
Tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa kwenye kila gram 100 ya mchaichai, kuna viondosha sumu ambavyo vina uwezo wa kuukinda mwili dhidi ya ugonjwa wa saratani. Mwaka 2006, timu ya watafiti kutoka Chuo kikuu cha Gurion, Israel waligundua mchaichai una uwezo wa kuua seli zinaweza kusababisha saratani.
-Husaidia umeng’enyaji wa chakula
Chai ya mchaichai hurahisisha utaratibu wa mmeng’enyo wa chakula na pia hutibu magonjwa ya kuhara na maumivu ya tumbo ikiwamo kujaa gesi na pia hurahisisha utaratibu wa kuondoa uchafu mwilini. Mafuta ya mchaichai yanasaidia kwenye mzunguko haswa kwa wanawake kuna wanawake huwa ni wakavu sana na hii husaidia sana kwa matumizi
Previous
Next Post »