Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania - TFF, Jamal Malinzi leo ameagana rasmi na aliyekua kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, mholanzi Mart Nooij.
Akiongea
na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Tansoma, Malinzi amesema
wameamua kuagana nae mbele ya vyombo ya habari kama iliyofanyika pia
wakati wa utambulisho wake wakati wa kuanza kazi.
“Mpira
wa miguu unachangamoto nyingi, watanzania tunasafari ndefu katika
mafanikio ndio maana TFF imeanza kuwekeza katika soka la vijana, sababu
ndio msingi wa kuwa na timu bora ya Taifa” alisema Malinzi.
Duniani
kote chimbuko la timu bora ni soka la vijana na watoto, tukiwa na
vijana wengi walioanza kucheza mpira katika umri mdogo wanapofikia umri
wa kuchezea timu ya Taifa tutakua na kikosi bora.
Nchi
za wenzetu inapofikia kocha kuita wachezaji wa timu ya Taifa anakuwa na
wigo mpana, kwetu sisi wachezaji wanocheza soka nje ya nchi
wanahesabika, hivyo ni lazima tuanze kuwekeza kwenye soka la vijana.
TFF
ilishaanza mkakati huo ndio maana kuna timu za U13, U15 ambazo zitakua
zikiingia kambini na kucheza michezo ya kirafiki ndani ya nje kwa lengo
la kupata uzoefu kabla ya kushiriki kuwania kufuzu kwa fainali za vijana
mwaka 2016.
Kikosi
cha U15 kinatarajiwa kufanya ziara mwezi Disemba mwaka huu katika nchi
za Malawi, Zambia, Zimbambwe, Botswana na Afrika Kusini, kisha mwakani
mwezi April 2016 kitaenda Rwanda, Burundi, Uganda na Kenya kucheza
michezo ya kirafiki.
Naye
Mart Nooij aliyekua kocha wa Taifa Stars, akiongea na waaandishi wa
habari alisema anawashukuru watanzania wote, serikali, wadau wa mpira wa
miguu nchini na TFF kwa sapoti waliyompatia wakati akiwa kocha mkuu wa
timu ya Taifa.
Nooij
alisema alifurahia maisha yake akiwa Tanzania kwa kipindi chote
alichokua akifundisha timu ya Taifa, lakini kwa sababu imefikia mwisho
wa ajira yake hana jinsi anaondoka, lakini ataendelea kuikumbuka
Tanzania na watanzania wote kila siku kwa ukarimu wao.
Wakati
huo huo Rais wa TFF. Jamal Malinzi amemtangaza Charles Mkwasa kuwa
kocha mpya wa Taifa Stars akisaidiwa na kocha Hemed Morocco, Mkwasa
ambaye ni kocha wa Yanga na Morocco kocha wa Mafunzo watafanya kazi kwa
kipindi cha miezi mitatu ambayo timu ya taifa itakua na michezo ya
kuwania kufuzu kwa CHAN na AFCON.
Malinzi
amesema uteuzi wa makocha hao wazawa umezingatia vigezo vya makocha wa
timu ya Taifa kuwa na leseni A ya ukocha kutoka CAF au zinazofanana
kutoka mashiriksho mengine duniani wanaozifanyia kazi, jambo ambalo
makocha hao wazawa wamekizi.
Kocha
Mkwasa atakua akipewa hudumu zote na masilahi (zikiwemo posho)
alizokuwa anapewa kocha aliyeondoka, pia amepewa nafasi ya kuchagua
benchi lake la ufundi la kufanya nalo kazi, hivyo nawaomba wadau wa
mpira wa miguu na watanzania kwa ujumla tuwape sapoti makocha hao
wazawa” aliongeza Malinzi”
Aidha
Kamati ya utendaji ya TFF Iimemteua Alhaj Ahmed Mgoyi kuwa mratibu wa
timu ya Taifa, lengo la uteuzi huo wa Mgoyi ni kuwa kiunganishi kati ya
kamati ya Utendaji na timu ya Taifa.
U15 Yaingia Kambini
Timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 ya Tanzania, imeingia
kambini jana na kuanza mazoezi leo katika uwanja wa Karume kujiandaa na
mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini U15 ya mkoa wa Mbeya siku ya
jumapili.
Kikosi
hicho kilicho chini ya makocha Bakari Shime na Peter Manyika kitacheza
mchezo huo kwa lengo la waalimu kupatawa fursa ya kuwaona vijana hao na
kuwaongeza wengine watakaoneka katika kikosi hicho.
U15
ni mpango wa TFF kuandaa kikosi kizuri chenye ubora kuelekea kuwania
kufuzu ka fainali za vijana Afrika mwaka 2017 zitakazofanyika nchini
Madagascar, ambapo vijana hao watakua na umri wa miaka 16 kufikia
mwakani wakati michezo ya kuwania kufuzu itakaponza mwezi Julai, 2016.
NB:
Kesho siku ya jumatano kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Mkwasa na
msaidizi wake Hemed Moroco wataongea na waandishi wa habari saa 5:30
asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume.
Waandishi wote wa habari mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.
Imetolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
EmoticonEmoticon