Kaimu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE)Dkt. Adolf
Rutayuga(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam(hawapo pichani)wakati wa kutangaza ubora wa elimu ya ufundi
inayotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo vitatu
na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.Kushoto ni Mkurugenzi wa Mitaala
wa baraza hilo Twilumba Mponzi na Msaidizi wa katibu Mtendaji Alex
Nkondola.
Wakurugenzi
wa Manejimenti ya NACTE wakiwa kwenye mkutano pamoja na waandishi wa
habari uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi inayotolewa na baraza
hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha hadhi
vyuo kumi na sita.
.Mwandishi
wa habari kutoka kituo cha EATV, Noah Laltaila akimuuliza swali Kaimu
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi (NACTE)Dkt. Adolf
Rutayuga kwenye mkutano uliohusu kutangaza ubora wa Elimu ya ufundi
inayotolewa na baraza hilo lilitangaza kuvifutia usajili vyuo vitatu na
kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
Baadhi
ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye mkutano wa
Baraza la Taifa la Elimu ya ufundi(NACTE) uliohusu kutangaza ubora wa
elimu unaotolewa na baraza hilo.Baraza hilo limevifuta usajili vyuo
vitatu na kuvishusha hadhi vyuo kumi na sita.
Katika
jitihada za kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini, Baraza la Taifa la
Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifutia usajili vyuo vitatu na kuvishusha
hadhi vyuo kumi na sita.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mtendaji
wa NACTE Dkt. Adolf B. Rutayuga alisema kuwa, hatua hiyo imefikiwa
baada ya vyuo husika kushindwa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na
NACTE.
“Kwa
kutumia Sheria ya Bunge Sura Na. 129 na Kanuni za Baraza za Usajili
(2001) na zile za Ithibati na Utambuzi (2001), mnamo tarehe 20 Februari
2015, Baraza lilitoa notisi ya siku 30 kwa taasisi na vyuo vilivyokiuka
taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya Usajili na Ithibati kupitia
taarifa yake kwa Umma. Notisi hii ililenga kuzipa taasisi na vyuo nafasi
ya kujitetea na kufanya marekebisho yaliyobainishwa,” alieleza.
Kaimu
Katibu Mtendaji huyo ambaye ni Mkurugenzi wa Ushauri na Malezi ya
Taasisi na Vyuo vya Ufundi NACTE aliwaambia waandishi wa habari kuwa,
Baraza linakiri kuwa taasisi na vyuo vingi vilivyopewa maelekezo ya
kufanya marekebisho vimechukua hatua mbalimbali za kurekebisha mapungufu
yabainishwa. Hata hivyo alisema hadi kufikia leo tarehe 24 Juni 2015
yaani siku 124 baada ya Notisi ya Baraza, kuna vyuo ambavyo havijachukua
hatua yoyote ya kurekebisha mapungufu yake.
“Baraza
limeamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kwa taasisi
na vyuo vyote vilivyoorodheshwa kwa makosa yafuatayo, moja kumalizika
kwa muda wa Usajili wa Awali (Preparatory Registration) na Usajili wa
Muda (Provisional Registration); pili kutoanza mchakato wa kupata
Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; tatu kumalizika kwa muda wa
Ithibati na kutochukuliwa hatua ya kuomba upya Ithibati
(re-affirmation); na nne taasisi na Vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa
mafunzo kwa sababu mbali mbali,” alifafanua
Vyuo
vilivyofutiwa usajili ni pamoja na Dar es Salaam College of Clinical
Medicine cha jijini Dar es Salaam kilichokuwa kimepatiwa usajili wa
awali, Ndatele School of Medical Laboratory Sciences cha Dar-es-Salaam
kilichokuwa kimepatiwa usajili wa awali na Institute for Information
Technology cha jijini Dar es Salaam pia chenye namba za usajili
REG/EOS/014.
Taassi/vyuo
vilivyoshushwa hadhi baada ya kushindwa kutiza mashart ni pamoja na
Sura Technologies – Dar es Salaam, Institute of Management and
Information Technology – Dar es Salaam, Techno Brain – Dar es Salaam,
Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi – Mbeya, Mbozi School
of Nursing – Mbeya, KCMC AMO Ophthalmology School – Moshi, KCMC AMO
Anaesthesia School – Moshi, Advanced Pediatrics Nursing KCMC – Moshi.
Vingine
ni, AMO Training Centre Tanga – Tanga, CATC – Songea, CATC –
Sumbawanga, COTC Maswa – Shinyanga, COTC – Musoma, Dental Therapists
Training Centre – Tanga, Ngudu School of Environmental Health Sciences –
Kwimba na KCMC AMO General School – Moshi.
EmoticonEmoticon