Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora kaimu kamanda wa
polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Juma Bwire amemtaja mutuhiwa wa
tukio hilo kwa jina la Masanja Mwinamila, ambaye aliangukia katika
mikono ya polisi kutokana na taarifa za wasamalia wema, na polisi kuweka
mtego.
Aidha kaimu kamanda wa polisi Juma Bwire amesema kuwa fedha alizo
taja kumuuza binti huyo, idadi imehifadhiwa isiwe kichocheo, huku akidai
kuwa, wanaendelea kumuhoji kama kuna watu anaoshirikiana nao.
Mama mzazi wa mtoto huyo aliyenusurika Magrethy Hamisi (miaka sita)
ambaye pia ni mlemavu wa ngozi, amesema kuwa, katika nyumba yao anaishi
na watoto wake kutokana na kufiwa na mmewe walivamiwa na watu waliokuwa
wameficha nyuso zao na kuanza kuwafukuza na kisha kumkamata mtoto huyo
na kutokomea naye.
Aidha kaimu kamanda Juma Bwire ameitaka jamii kutoa ushirikiano
pale wanapobaini watu wanaosababisha walemavu wa ngozi kuishi kwa
wasiwasi ili kukomesha vitendo vya ukatili.
EmoticonEmoticon