MJUMITA WAZINDUA WIMBO WA MKUHUMI ULIOIMBWA NA MPOTO, AFANDE SELE NA DAYNA


WATANZANIA wametakiwa kuwatumia wasanii katika kufikisha ujumbe wa masuala muhimu ya kijamii kwakuwa wasanii hao wanamvuto mkubwa kwa wananchi.



Hayo yalisema jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa wimbo maalum wa kuhamasisha utunzaji wa mazingira  uliojulikana kama  ‘Mkuhumi’.

Wimbo huo ulioimbwa na wanamuziki wa kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’, Dayna Nyange pamoja na msanii nguli wa kughani mashairi Afrika Mashariki, Mrisho Mpoto maarufu kama ‘Mjomba’.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa wimbo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi alisema, wameamua kuwatumia wasanii hao kwa kuwa ni rahisi kufikisha ujumbe kwa jamii.

Alisema lengo kuu la wimbo huo ni kuwahamasisha wananchi kutunza mazingira ili waweze kunufaika na Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi), kupitia fedha zinazotolewa na nchi zenye viwanda.

“Watu wengi tunapoenda kusikiliza muziki kuliko kusoma, kwa maana hiyo kama tungeweka elimu hii kwenye vipeperushi isingekuwa rahisi kwa watu wote kupata ujumbe, lakini tunategemea kupitia muziki huu tutawafgikia watu wengi,” alisema.

Alisema wimbo huo umetayarishwa chini ya usimamizi wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Mkuhumi ili kuwafikia wadau ili kwa pamoja waweze kuchukua tahadhari na kupunguza shughuli zinazochangia kutokea kwa mabadiliko ya tabia nchi.

“Kupitia wimbo huu jamii itapata uelewa utakaosaidia kuhamasisha jamiikutumia rasilimali za misitu kwa njia ya uendelevu na kujipatia faida,” alisema Njaidi.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Mjumbe wa Kikosi kazi cha Mkuhumi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Julitha Masanja ambaye alipongeza kazi nzuri inayofanywa na taasisi hiyo ya Mjumita. 

“ Mjumita inapaswa kuungwa mkono kwa nguvu zote kwani inasaidia kutunza misitu ya asili ambayo imekuwa na changamoto kutokan ana shughuli za binadamu,”alisema Masanja.


Mjumbe wa kikosi Kazi cha Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi),Kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,  Julitha Masanja (kushoto) akiwa ameshikilia CD na DVD alizozizindua jua ambazo zina nyimbo maalum wa Mkuhumi ambao hupambana na uharibifu wa mazingira Dar es Salaam jana. Pamojanae ni Mkurugenzi wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu (Mjumita), Rahima Njaidi
 Mjumbe wa kikosi Kazi cha Kupunguza Uzalishaji wa Hewa ya Ukaa kutokana na ukataji na uharibifu wa Misitu (Mkuhumi),Kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira,  Julitha Masanja akikabidhi DvD kwa wanahabari,
 Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili nchini, Bettie Luwuge akifafanua jambo juu ya mradi huo.
 Mtaalam wa IRA, Edmund Mabhuye akiwasilisha mada juu ya mabadiliako ya tabia nchi na ongezeko la hewa ukaa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi akizungumzia uzinduzi huo Dar es Salaam leo.
Wanahabari n mbalimbali wa kifuatilia maelezo juu ya miradi ya hiyo ya uhifadhi mazingira.
Previous
Next Post »