·
MTU MMOJA AUAWA KWA KUKATWA PANGA NA WANANCHI
KWA TUHUMA ZA WIZI.
·
MTU MMOJA AKUTWA AMEUAWA NA WATU WASIOFAHAMIKA
NA MWILI WAKE UKIWA NA MAJERAHA YA KUCHOMWA MOTO.
·
MTEMBEA KWA MIGUU AMEKUFA MARA BAADA YA KUGONGWA
NA GARI JIJINI MBEYA.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI
YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 35-40, ALIUAWA KWA KUKATWA
MAPANGA MWILINI NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI HUKO ENEO LA
MACHINJIONI – VETA JIJINI MBEYA.
MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA HUKO KATIKA ENEO LA
MACHINJIONI – VETA, KATA YA SAE, TARAFA YA IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE 24.05.2015 MAJIRA YA SAA 20:30 USIKU.
INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI TUHUMA ZA
WIZI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA, UPELELEZI
UNAENDELEA ILI KUWABAINI NA KUWAKAMATAWAHUSIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE,
JINSI YA KIUME, UMRI KATI YA MIAKA 18-22, ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA SEHEMU
MBALIMBALI ZA MWILI WAKE NA WATU WASIOFAHAMIKA NA KUUNGUZWA MOTO SEHEMU ZA
MAPAJA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 24.05.2015 MAJIRA YA SAA 19:20 JIONI HUKO KATIKA MSITU WA SHULE YA MSINGI MAPOROMOKO, KATA
NA TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA TUKIO BADO KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. UPELELEZI UNAENDELEA ILI KUWABAINI NA
KUWAKAMATAWAHUSIKA.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI NYIGESA R. WANKYO
ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAJENGE TABIA YA KUWAFIKISHA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTEMBEA KWA MIGUU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA MOJA LA SUBIRA, UMRI KATI YA MIAKA 25-30,
MKAZI WA NZOVWE ALIFARIKI PAPO HAPO
BAADA YA KUGONGWA NA GARI ISIYOFAHAMIKA NAMBA ZAKE ZA USAJILI WALA DEREVA WAKE.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 24.05.2015 MAJIRA YA SAA
20:50 USIKU HUKO ENEO LA OIL-COM STENDI KUU, KATA NA TARAFA YA SISIMBA,
JIJI NA MKOA WA MBEYA.
DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA AJALI. CHANZO
CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA
MBEYA, UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA DEREVA ALIYEHUSIKA
KATIKA TUKIO HILI.
[NYIGESA R.
WANKYO – ACP]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon