JESHI LA POLISI MKOA WA
MBEYA LINAWATAKA WANANCHI WOTE WA MKOA WA MBEYA KUSHEREKEA KWA AMANI SIKUKUU YA
PASAKA BILA KUWEPO KWA VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI
ZIPO KAMATI ZA ULINZI NA
USALAMA ZA NYUMBA ZA IBADA, TUNAPENDA KUWAKUMBUSHA VIONGOZI WA NYUMBA HIZO ZA
IBADA KUIMARISHA ULINZI NA USALAMA WA NYUMBA HIZO, WAUMINI NA MALI ZAO KAMA
VILE VYOMBO VYAO VYA USAFIRI WAKATI WA IBADA ZA MKESHA WA PASAKA.
KWA WAMILIKI WA KUMBI ZA
STAREHE, TUNAWAKUMBUSHA KUWEKA WALINZI WA NDANI YA UKUMBI, KUZINGATIA MUDA WA
KUANZA NA KUFUNGA KUMBI ZAO PAMOJA NA KUZINGATIA UWEZO WA UKUMBI UKILINGANISHA
NA IDADI YA WATU.
KWA WATUMIAJI WA VYOMBO VYA
MOTO WAWE MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA SHERIA,
KANUNI NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI. KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KAMA
VILE WATEMBEA KWA MIGUU, WAENDESHA BAISKELI NA WASUKUMA MIKOKOTE KUWA MAKINI
KATIKA MATUMIZI YA BARABARA IKIWA NI PAMOJA NA KUVUKA MAENEO RASMI YA KUVUKIA
PAMOJA NA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA.
PIA JESHI LA POLISI
LINAWAKUMBUSHA WAZAZI NA WALEZI KUWEKA UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WAO
KATIKA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU IKIWA NI PAMOJA NA KUHAKIKISHA MTOTO ANAKUWA
CHINI YA UANGALIZI WA MTU MZIMA WAKATI WA KUTOKA NYUMBANI KUELEKEA NYUMBA YA
IBADA AU MAENEO YA SHEREHE. KUHUSU DISCO TOTO, HATURUHUSU WATOTO KUCHEZA MUZIKI
KATIKA KUMBI NA NI VYEMA WAKACHEZA KWENYE MAENEO YALIYOWAZI KWA AJILI YA
USALAMA WAO. PIA TUNASHAURI WANANCHI, KUACHA WAANGALIZI KATIKA NYUMBA ZAO WANAPOTOKA
KUELEKEA KATIKA IBADA AU SEHEMU ZA STAREHE ILI KUEPUKA MATUKIO YA UVUNJAJI,
WIZI, UDOKOZI NA UPOTEVU WA MALI.
KWA UPANDE WA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA, TUMEJIPANDA VYEMA KUFANYA DORIA ZA MIGUU, MAGARI, NA
PIKIPIKI KATIKA MAENEO YOTE KUZUNGUKA JIJI LA MBEYA NA VIUNGA VYAKE. PIA KWA
KUSHIRIKIA NA KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA ZA NYUMBA ZA IBADA, PIA TUMEZITAMBUA
NYUMBA ZA IBADA ZITAKAZOFANYA IBADA ZA MKESHA WA PASAKA NA TUTAWEKA ASKARI KATIKA
NYUMBA HIZO KWA KUSHIRIKIANA KUFANYA KAZI PAMOJA NA KAMATI HIZO HASA KATIKA
IBADA ZA MKESHA WA PASAKA. PIA ASKARI WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI
WATAKUWEPO KATIKA MAENEO YOTE KUHAKIKISHA USALAMA WA WATUMIAJI WA BARABARA NA
KUDHIBITI MADEREVA WASIOFUATA NA KUTII SHERIA ZA USALAMA BARABARANI.
AIDHA TUNAPENDA KUWAAMBIA WANANCHI
WAZINGATIE USEMI HUU “USALAMA KWANZA,
KWANI MAHALI POPOTE PENYE USALAMA, AMANI NA UTULIVU NDIPO MAENDELEO YA ENEO
HUSIKA YANAKUWEPO. BILA USALAMA, HUTOWEZA KWENDA KUABUDU KWENYE NYUMBA ZA
IBADA, HUTOWEZA KWENDA KULIMA, HUTOWEZA KUFANYA BIASHARA, KWENDA HOSPITALINI
KUTIBU AU KUTIBIWA, KUSAFIRI BILA HOFU NAKADHALIKA. KWA MAANA HIYO, USALAMA NI
KITU CHA MUHIMU KWA MAENDELEO YA MAISHA YETU, MKOA WETU NA TAIFA LETU.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA PASAKA YENYE AMANI NA UTULIVU.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon