Ajali hii imetokea eneo la iyovi lililopo safu ya Milima ya Uduzungwa kando ya Mto Ruaha Tarehe 12/04/2015 majira ya Saa mbili asubuhi bus T.373 BAH Kampuni ya Nganga Express lililokuwa linatokea Kilombero kwenda Mbeya likiwa kwenye mistari ya barabarani ya katazo likiwa kwenye milima huo likiwa kwenye mwendo kasi, gari hilo liligongana na Mistubishi Fuso T.164 BKG iliyokuwa imebeba matikiti kisha kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu 15 kutoka kwenye basi na 3 kutoka kwenye Fuso na majeruhi 10 ,wanawake 4 na wanaume 6 ,ambapo wanne wamelazwa Hospitali ya ST.Kizito Mikumi na Sita Hospitari ya Mtandika Iringa.
Aidha kwenye bus kulikuwa kuna pikipiki iliyoungua ambayo inawezekana ndio iliyosababisha moto kuwaka na kuunguza bus na fuso.
EmoticonEmoticon