Sim no,0755683295/Watsap, Emal@yusuphngahala@gmail.com, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala, Instagram @mwalim_yuu.
SEHEMU YA KUMI NA MOJA.
Tulipoishia kisha nikatoa amri ya kumsogelea kwa karibu. Tulisogea kwa tahadhari ambapo yeye alikua hajashtuka bado. Wakati natoa amri ya kumshambulia ghafla yule mtu______Endelea...Alifunua kitu kama mfuniko na kuzama pale chini. Nilijilaumu kwanini nilichelewa kutoa amri. Nikawaamrisha wenzangu kusogea pale kwa tahadhari. Tulisonga kwa kutembelea tumbo ili tutoingia kirahisi kwenye "target" za majambazi. Baada ya kufika pale mimi nikasimama na kujitoa muhananga. Nikafunua ule mfuniko. Nikakutana na ngazi zimeshuka chini. Nikawaambia wenzangu hakuna jinsi lazima tuingie. Nilianza mimi lakini wakati naingia kwa nyuma nilihisi kuna afande mmoja anatumia simu ya kawaida wakati hairuhusiwi.
Nilimwona kajisahau sana alionekana kama anatuma SMS sehemu. Tena alikua mwenye wasiwasi fulani. Nilishuku kitu ila nikajibia nitamkamata tuu subiri. Basi nikaanza kushuka ngazi. Na maafande wengine wakafuata. Tulishuka huku bunduki zikiwa tayari. Tulifika chini na kukuta kuna eneo kubwa na taa zikiwaka na kutoa mwanga kama mchana. Ilikua kama vile sebule ya watu kulikua na viti, tv flat screen, kubwa sana na pia palipambwa haswaa. Baada ya kua wote tumeingia nikaamuru kutawanyika na kila ukionacho mbele halali yako. Tukagawanyika mle na kuanza kutafuta watu mle ndani. Niliingia chumba cha kwanza nilikutana ni vitu vya ajabu sana.
Nilikutana pakti za madawa ya kulevya zikiwa tayari zimeandaliwa. Nikawaaita maaskari kadhaa kwa "redio call" kuja pale wakaja nikawaamuru kulinda pale. Nikasonga mbele huko sasa nilikoingia ndiko ilikua shida. Kwanza nilikuta watu wamelazwa pamoja wengi kwelikweli. Sikujua kama ni wazima au laa. Lakini kwa jinsi walivolazwa walikua wamekufa kwasababu walikua wamelaliana ovyo. Wakati nawasogelea niwaone vizuri pembeni kulikua na majeneza kama manne hivi. Niliona yamefunuliwa na ndani mlikua na watu. Nikajua ni maiti. Lakini wakati nataka kuanza kukagua zile maiti. Ghafla watu wa kwenye majeneza mawili wakasimama.
Kumbe hazikua maiti bali walinzi wa mule. Walianza kwa kunizunguka huku wakinielekezea bastola. Nilijihisi mwisho wangu umekaribia. Nikaingiwa na woga. Lakini nilipokumbuka maneno ya mke wangu yalinitia nguvu mpya. Nikakumbuka depo, Nikaona njia pekee ni kujifanya nimeshindwa kisha naruka "tiktaka ya kushtukiza. Ashukuriwe Mungu nlifanikiwa ambapo niliwaangusha wote. Sikua na kingine zaidi ya kuwapiga risasi. Wakati nageuka akainuka wa jeneza la tatu. Huyu kabla hajanipiga alipigwa na kitu kizito kichwani akaanguka.
Wakati naangalia nani aliyempiga sikuamini macho yangu. Alikua ni Anthony yule mtoto wa Marehemu bosi wangu. Kwa kua nilijua na jeneza lile lingine ni mlinzi nikaliwahi. Nilifunika kishanikafyatulia risasi bila kikomo. Nikamchukua Anthony na kumtoa sebuleni pale nikamkabidhi afande mmoja. Kisha nikarudi pale. Maiti zilikua nyingi huku zikiwa zimefumuliwa matumbo huku zikionekana kama zimeshonwa. Nilijua tuu walikua wakizitumia kusafirishia madawa ya kulevya.
Niliumia sana kwakweli. Watanzania tumefika wapi. Mtu kwasababu ya pesa anampasua mwenzie na kumpakia madawa kisha anamshona kama gunia. Kweli? Kisha unapita barabarani eti umebeba maiti kwanini lakini tumekua wanyama. Baada ya kutafuta kote hatukuona mtu. Zaidi miili ya wale madaktari wanne ilikutwa imeuawa kikatili na kukatwa vichwa. Hii ilipatikana chumba fulani aliyegundua alikua Peris.
Baada ya kuhakikisha hakuna watu tukaanza kujadili tufanyeje. Makubaliano ilikua ni kubeba zile maiti za mle zote kisha tumwage petrol tuchome mle. Maana ilionekana ile ni sehemu yao kubwa maficho. Basi baada ya maafande kadhaa kutoa maiti nje walikuja na petrol kisha tukamwaga mle na tukapanda hadi ngazi ya juu kabsa hapo pia tukamwaga mafuta na kuwasha moto.
Tulifunika pale na kuhakikisha kua moto usingeweza kutoka nje. Tulipakia maiti zote kwenye gari na kuondoka eneo lile. Wakati tumefika kituoni nilimwita kwa ghafla yule afande niliyemuhisi anafanya kitu kwenye simu. Alipofika nikamwamuru anipe simu. Alionekana kutetemeka sana. Aliponipa nikamwambia atoke. Kisha nikaanza kuipekua. Mungu wangu niliona Jumbe nyingi kweli akiwa anawasiliana na majambazi. na ya mwisho kutuma yeye aliandika "KIMBIENI KIKOSI NI KIKUBWA NA CHOTE KINAINGIA HAMTAWEZA KUPAMBANA TUKO HAPA KWENYE NGAZI" nyingine pia nikaona alikua anatoa maelekezo mahali siraha za jeshi zinahifadhiwa. Haaa!! Nilipatwa na mshangao nikaamua kumfuata lakini wakati natoka nikawaona polisi wamemzunguka.
Kumbe aliamua kujiua kwa kujipiga risasi kichwani. Nililaumu sana kuona afande analisaliti jeshi la polisi. Na alijiua kukwepa kuhojiwa. Wakati natafakari nini cha kufanya nikasikia simu yangu inaita. Baada ya kuangalia ilikua namba ngeni. Baada ya kupokea nikasikia sauti ikilalamika. Kuna uvamizi umetoka benki ya NMB tawi la mwenge. watu wenye silaha wanaua watu ovyo. Kisha simu ikakatika. Nilipopiga kupata maelezo zaidi haikupatikana. Nikaamuru kikosi mara moja kuwahi eneo hilo.
Baada ya kufika tulipoelekezwa tukashangaa ile benki hali ni shwari na hakuna dalili za uvamizi. Nilimfuata meneja ambaye alithibitisha kua hakuna uvamizi. Nikaipiga ile namba haikupatikana. Nikaamua kuangalia jina kwa njia ya M-PESA ndipo nikaona imesajiliwa kwa jina Zabroni Makweka. Nikajua tuu ni mchezo tumechezewa. Nikaamuru kikosi kurudi kituoni . Baada ya kufika kituoni hali ilikua tofauti kabsa na tulivyoacha. Kwanza askari kadhaa walikua wameuawa kikakatili sana. nadhani kwa askari waliokua wamebaki pale walikua kama 15 hivi lakini waliobaki hai walikua watatu tuu.
Nao hali zao zilikua mbaya sana.Mkuu wa kituo alikua akitapatapa tuu. Nilijiona mjinga na niliyekurupuka kutoa amri ya kwenda kupambana na majambazi kumbe nyuma naacha mauaji. Nilisikitika sana. Wakati naendelea kukagua miili ya maaskari kuna ujumbe uliingia kwenye simu yangu. Niliitoa na kuangalia nani mtumaji. Chaajabu ni kua sikua "nimesave" namba ya Zabroni lakini jina lilitokeza Zabroni. Nilishtuka sana nikaufungua nao ulisomeka hiviii________________________
Sent from Huawei Mobile
EmoticonEmoticon