MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no,+255755683295/Watsap,Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala. Email,yusuphngahala@gmail.com. Instagram @mwalim_yuu.
SEHEMU YA NNE.
Tulipoishia Nikakuta imeenda chooni na nilipofungua mlango wa choo. Nikakutana na mwili wa Mkuu akiwa amekatwa kichwa. Woga ulianza kuniingia nikageuka nyuma nikaona_____Endelea......... Kisu kilikua na damu kiasi. Nikashuku huenda ndicho kilichotumika kutenganisha kichwa cha mkuu wangu wa kazi.Nikaamua kuzunguka nyumba yote kuona kama kuna usalama. Nilianza kutembea kwa kujihami kuelekea chumba hadi chumba. Niliingia chumba ambacho nadhani ilikua ni chumbani kwa mkuu. Nilikutana na mwili wa mwanamke umekatwa mikono yote. Pia kichwa kilikua kimetenganishwa na kiwiliwili. Ulikua ni ukatili wa ajabu sana. Pembeni nilimwona mtoto akiwa amefungwa mdomo na mikono na miguu yake. Alikua akinifahamu sana. Alinitazama kwa jicho la huzuni nachozi yalikua yakimtoka bila kikomo mtoto wa mkuu wangu wa kazi. Alikua ni mdogo sana. Masikini majambazi hawana huruma kumfunga ivi mtoto wa miaka mitano.
Nilimfuata mtoto na kumfungulia alinirukia na kunikumbatia. Nilimhurumia sana. Basi nikamshusha na kutoka nje ili nione kama usalama upo. Baada ya kuhakikisha usalama kiasi. Nikapiga simu kituoni ili waje pale mara moja. Baada ya mda mchache wakafika. Basi wakachukua ile miili. Mkuu wa kwetu na Mke wake. Yule mtoto alikua bado ana woga nilimbeba.
Baada ya kua wamebeba kila kilichohitajika. Ikiwa ni pamoja na visu vile naile mikono ya yule mke wa Boss, pamoja na kichwa chake. Pale nikaamuru wabaki askari kadhaa kwaajili ya Doria. Tulifika kituoni nikaitisha kikao cha dharura na kuwaambia wenzangu. Hii ni hatari ikiwa mpaka boss wetu mlinda usalama wetu, na wa raia anauawa hii imepitiliza. Tunaipeleka wapi Tanzania hii. Sasa bila kusikiliza serikali imeamua nini. Nataka ndani ya wiki moja tuwatie nguvuni waliohusika na mauwaji ya Afande na mkewe.
Nikawaamuru watawanyike na kazi ianze mara moja, basi mimi nikampeleka yule mtoto nyumbani. Mke wangu hakua na tatizo hata kidogo. Nikawasiliana ndugu wa marehemu wakafanya taratibu za mazishi na kuwazika. Nakumbuka ilikua siku ya Alhamisi ikiwa imebaki siku moja. Ripoti ya majambazi waliohusika kukamatwa. Nilikua nimechoka kiasi nikaamua kwenda Nyumbani mara moja.
Wakati nakaribia nyumbani nilimwona mtu akiwa amesima na yule mtoto wa marehemu. Alikua kama akimpa kitu hivi. Ghafla alipoiona gari yangu akamwachia mtoto na kutoka mbio. Niliongeza spidi kiasi nikashuka na kukuta kashapotea. Nikarudi kwa mtoto ambapo nilishangaa akisema. Anko umeshabadilisha nguo sasahivi. Nilishtuka nikamwuliza Yule alikua hapa ni nani. Akajibu ni wewe anko uliniletea biskuti hizi. Nikasema hapana mi ndo nafika akajibu hapana Umeleta biskuti hizi. Kuona vile tayari nikaingiwa na wasiwasi nikamwambia sasa nipe hizo biskuti nikupe hizi huku.
Nikaingia kwenye gari nikachukua pakti na kumpa. Zile alizopewa na mtu aliyedai ni mimi nikazichukua. Baada ya kuziangalia nikagundua kitu.Nikamwambia ingia ndani na usitoke sawa ee? Akajibu sawa. Nikazipeleka kwa daktari mmoja jirani. Akazipima na kusema ile ni sumu kali sana. Akadai inadhuru hata kwa kuishika hebu kamlete mtoto haraka. Nilikimbia nyumbani na kukuta kweli Yule mtoto ametoka vitu kama malengelenge mikononi. Nilimchukua na kumkimbiza kwa daktri.
Alimfunga bandeji na kuniasa kua makini na mtoto. Mimi nilisalimika kwasabu nilikua nimevaa "groves" Nikawa najiuliza ni nani huyu anayenisumbua kichwa kiasi hiki? Je alitaka kumwua Yule mtoto kwasababu gani? Na pia yule mtoto alisema ni mimi. Je ni yule mtu ambae siku zote akifanya jambo mimi ndo huonekana nahusika? Ni nani huyu? Nikamchukua mtoto yule na kurudi nyumbani.
Nilipofika nyumbani nilikua sijatulia kabsa. Kwani nilianza kuhisi kua hata kwangu pia si salama. Nikasema hivi kwanini n aishi kwa mashaka. Afisa mpelelezi wa Jeshi la polisi. Mlinzi wa raia na mali zake kwanini niishi kwa mashaka. Je wananchi wa kawaida itakuaje? Nikasema hapana hii imezidi sasa. Lazima tusimame imara kupigania usalama wa nchi yetu. Kwanini majambazi wasumbue vichwa vyetu? Kwanini majambazi waharibu sifa ya Tanzania?
Nikasema haiwezekani. Nikatoka na kuelekea kituoni. Huko nikawaita maafande na kuwataarifu kua makini. Baada ya maongezi nikatoka na kuelekea kituo chajirani. Nilikua naenda kuongea maswala nyeti kidogo. Baada ya maongezi nikawa narudi Nyumbani. Kwa mbali nikamwona mtu aliyekua kama anafanana na mimi anavuka barabara. Nikaona "Yes" nimemwona mbaya wangu. Nikaegesha gari pembeni nikashuka na kuanza kumfukuzia kwa nyuma. Nilipomkaribia mara ghafla________________________
EmoticonEmoticon