SIMULIZI YA KUSISIMUA-NANI KACHUKUA SURA YANGU?



MTUNZI NA MWANDISHI-MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.

Sim no,+255755683295/Watsap,

Facebook.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala,Email- yusuphngahala@gmail.com,instagram@mwalim_yuu.

SEHEMU YA TATU.
Tulipoishia Aliongea huku akinitaka nikae katikati nihojiwe juu ya tukio lile. Huku afisa mzima nikionekana naua watu. Baada ya kukaa maswali yalianza hivi____Endelea......Afande ushahidi wa mkanda wa video unaonyesha wewe ukihusika kuua watu pale sheli, Je una upingamizi? Nikajibu ndiyo mkuu. Si kweli kua mimi nilishiriki katika uvamizi. Mimi ndiye niliongoza vikosi vyote mara baada ya kuwasili. Mimi ndiye niliua jambazi mmoja kati ya wale wawili.

Nikiwa naendelea kuongea kuna afande mwingine akanyoosha mkono. Alikua ni kutoka kituo kingine. Akaruhusiwa kuongea naye akaanza kwa kusema. Wakuu hili swala liangaliwe kwa jicho la tatu. Yule anayeonekana kuua watu na kupora pesa hakuvaa sare za jeshi. Afande Yuu alikua na sare. Mimi na maafande wengine tulikua na Afande yuu hatukumwona kuingia ndani ya sheli. Mwingine akadakia ni kweli mimi hadi tukio linaisha tulikua na Afande karibu. Maelezo kama hayo yalitolewa na askari zaidi ya kumi. Kisha mkuu wangu wa kazi akaingilia kwa kusema.

Ndugu zangu Afande Yuu ni afisa mpelelezi mwaminifu sana. Najivunia kuwa naye. Sioni kuhusika kwake kwani kwa mujibu wa maelezo ya maafande wengine wanakanusha. Hata mimi nawaunga mkono Yuu namjua na naamini hawezi kusaliti jeshi la polisi. Swala la msingi ni kuangalia huenda majambazi wanatuzidi ujanja wa kiteknolojia. Tulifikirie upya. Alipomaliza kuongea kidogo roho yangu ikaanza kutulia. Nikaona hata nguvu kubwa niliyokua nimejiandaa kujitetea ilikua kazi bure.

Nilitetewa na maafande wenzangu, na zaidi mkuu wangu wa kazi. Hali ile kuna baadhi haikuwafurahisha kabsa. Nyuso zao zilionyesha kua hawakufurahia. Basi maamuzi yakatolewa ya kua wateuliwe maafande 15, angalau kila kituo wawili ili kufuatilia swala lile na waje na ufumbuzi. Basi Tukaambiwa turudi kuendelea na kazi. Nilimshukuru Mungu na kuondoka zangu na kurudi ofisini. Nilikumbuka pia nina kesi zisizopungua nne za kupeleleza. Zikiwemo zile mbili za uvamizi wa benki na sheli kule ubungo.

Kichwa kilikua kimejaa mawazo. Nilikua nawaza jinsi ya kukabiliana na yule mtu anayeonekana kuua. Kisha mimi naonekana ni muuaji. Nilikua najiuliza je huyu jambazi ni kwamba nafanana naye tuu? Hapana si kwa kufanana vile mbona hata mimi niliona picha ni mimi yule. Je anaweza akawa anatumia sura ya bandia? Hapana hata mwili uko sawa na wangu. Ni ujuzi gani anatumia? Au ni jini? Hapana siamini ushirikina mimi hata kidogo. Sasa ni nini? Nachafuliwa na "CV'' yangu inaharibika.

Nilijiuliza maswali mengi sana bila majibu. Nikajisemea leo nimetetewa na wenzangu. Je ikija kutokea hakuna utetezi itakuaje? Nikajikuta naongea mle ofisini kwa sauti kuu huku nikigonga meza "Hard no" Haiwezekani. Afisa nachezewa sasa hawa maafande wadogo itakuaje? "I must do something" Nikaamua kwa mda ule niende nyumbani kupumzika kisha asubuhi nione naanzia wapi kazi yangu.

Wakati natoka afande Peris akaniuliza mkuu unaonekana hauko sawa nini tatizo. Nikamjibu sijisikii vizuri acha nikapumzishe akili. Basi akasema kwa ninavyokuona naomba nikusindikize mkuu. Nilimpenda sana Peris alikua na roho nzuri sana. Nilimkubalia nikampa funguo ya gari. Akaniendesha njiani tuliongea mambo mengi sana. Alinipa pole kwa mkasa ulionikuta. Nilimshukuru sana lakini pia nikamsisitiza juu ya kukamata majambazi. Alisema mkuu tutajitahidi usijali. Basi tulifika nyumbani kwangu Peris akaaga anarudi ofisini. Akanikabidhi funguo na kuondoka zake.

Niliingia ndani nikamkuta mke wangu na mwanangu wamepumzika. Walikua wakiangalia "TV" Nikamkumbatia mke wangu na kumbusu. Nikambusu mwanangu kama salamu kisha nikamwangalia mke wangu. Alianza kwa swali enhe! vipi mbona leo mapema? Nikamjibu mke wangu naomba n aomba kwanza nikalale nipumzike mana hapa hali siyo nzuri. Akili imesimama. Akajibu aaaah! pole jamani mume wangu. Nikajibu ahsante. Akasema haya kalale baba. Nikaingia ndani na kulala. Mda ukasonga nilishtuka usiku baada ya kuamka na kula na shuhuli zote kwisha tukalala na mke wangu.

Nilimsimlia kila kitu kilichotokea kazini alinihurumia sana. Basi sikua na ujanja nikamwambia najitahidi kukabiliana na hilo. Baada ya maongezi marefu tukalala. Asubuhi kulipokucha nikaamka na ari mpya. Nilikua nimeanza kuona naanzia wapi kushughulika na lile swala. Nilifika ofisini kisha nikaomba mafaili ya majambazi sugu wote. Niliyapitia kwa uangalifu sana. Pia nilikua napekua na kompyuta mle ndani. Mara kuna picha kadhaa nikaziona mle kwenye kompyuta. Picha zilikua zangu. Zilionyesha jina la Zabroni makweka. Nilishtuka sana. Baada ya kuzifuatilia nikagundua ile kesi ilikua inafuatiliwa na kupelelezwa na Afande mmoja wa pale kazini jina lilikua geni na sikua namfahamu.

Nikatoka kumulizia Juma kama anamfahamu aliyekua anampeleleza Zabroni Makweka. Juma akasema kwasasa ile kesi hajapewa mtu ila Aliyekua kaishikilia aliuawa na watu wasiojulikana. Nikiwa naongea naye simu yangu ikaita. Alikua ni mkuu anapiga simu. Nikapokea nikamsikia akisema njoo nyumbani kwangu haraka. Nilimwambia Juma narudi. Nikachukua pikipiki na kuwahi. Nilipofika nilimwona mtu anawasha pikipiki aina ya baja na kuondoka.

Sikumtilia manani mi nikaingia ndani. Na nilipofika sebuleni nilikutana na damu zimetapakaa. Nilishtuka sana nikatoa bastora kujihami kisha nikawa naifuata michirizi ya damu. Nikakuta imeenda chooni na nilipofungua mlango wa choo. Nikakutana na mwili wa Mkuu akiwa amekatwa kichwa. Woga ulianza kuniingia nikageuka nyuma nikaona_______________________
__________________________________________________________________________________________________________________________________________________________Je Afande Yuu aliona nini? Ungana naye sehemu ya 4 ujue hilo. Kwa lolote mcheki Yuu kwa 0755683295/Watsap, Fb.com/Mwalimu Yusuph Abel Ng'ahala. Email,yusuphngahala@gmail.com. Instagram@mwalim_yuu. Naipenda Tanzania, Nawapenda watz, Nawapenda woteeee.
Previous
Next Post »