MTUNZI NA MWANDISHI MWL YUSUPH ABEL NG'AHALA.
Sim no, 0755683295/Watsap. Instagram@ mwalim_yuu.
SEHEMU YA KWANZA.
Kwanza naomba nianze kwa kujitambulisha. Kwa majina yangu naitwa Yusuph Abel Ng'ahala maarufu kama Afande Yuu. Nilizaliwa Iringa na kusoma Shule ya msingi Luduga huko njombe na sekondari nikasoma Ivumwe huko Mbeya. Nilisoma sangu elimu ya "Advince", na kujiunga na chuo cha Dar es salaam. Baada ya kuhitimu masomo yangu nilijiunga na Jeshi la polisi ambapo tulienda depo kwa mda wa miezi sita. Baada ya kutoka depo kwa kua nilikua na elimu kiwango cha degree nilipangiwa kituo cha kazi huko Mwanza huku nikiwa na kacheo kiasi.
Nilifanya kazi huko mwanza kwa miaka mitatu kisha nikahamishiwa Dar es salaam. Kazi yangu niliifanya kwa ufanisi sana hadi nikabadilishwa kitengo na sasa nikawa Afisa upelelezi mkoa wa Dar es salaam. Nilikua najisikia furaha sana nilikua naona serikali inatambua mchango wangu katika kulinda raia na mali zao. Mke wangu na wanangu walikua wakinifuarahia sana kutokana na mafanikio yangu ya kazi. Hata mimi nilikua najiona mwenye bahati sana.
Nakumbuka kuna siku ulitokea uvamizi banki kuu. Kuna majambazi walikua wamevamia eneo lile. Mkuu wangu wa kazi akaniamuru nipeleke vikosi kadhaa. Bila kuchelewa nikatii amri mara moja na kwenda pale "BOT" na kuanza kufyatuliana risasi na majambazi. Tulikua tumejipanga vilivyo. Tulifanikiwa kuwatoa nao wakapotea kwa bahati mbaya hatukuwakamata.
Hatukulaumu sana kwasababu tulifanikiwa kulinda usalama wa banki kuu. Tulirudi ofisini mkuu wa kazi akatupongeza. Mimi akaniita ofini kwake baada ya kwenda akanambia, Afande Yuu mmefanya kazi nzuri lakini nakuomba nitakupa maaskari wawili nahitaji hawa majambazi wakamatwe, Fanyeni upelelezi wa kina na muhakikishe tunawatia nguvuni sawa? Nikajibu sawa mkuu. Basi akawaita Afande Peris na Afande Juma kisha akasema utakua nao hawa. Nawatakia kazi njema.
Baada ya siku kadhaa kupita mi nikaanza upelelezi wangu. Nilianza kwa kwenda pale BOT na kuomba picha zilizopigwa siku ya uvamizi. Nilikabidhiwa sikuzikagua na kurudi ofisini. Nikazihifadhi. Nikakumbuka pia siku ile kuna siraha kadhaa waliziangusha zikaokotwa nikamfuata afande Miraji ndo alikua nazo. Bila hiyana alinipa. Nikarudi ofisini na kuanza kukagua zile picha za uvamizi. Hapo utata ukaanza. kuna picha nilikua naiona nikawa naishangaa na kua kama nisiyeamini ninachokiona mbele ya macho yangu.
Ilikua ni mtu kavaa kombati za jeshi la wanachi JWTZ akiwa anaonekana kwenye kundi la majambazi. Chaajabu kila nilipoiangalia ile sura ilikua ni yangu. Kichwa kiakaanza kuuma. Sasa mimi kwenye kundi la majambazi nimeingiaje? Na sijawahi kua na nguo za JWTZ sasa hii ni nini jamani? Nikiwa nazishangaa zile picha za majambazi aliingia mkuu wangu wa kazi. Nilizigeuzia picha kwa chini kisha nikamkaribisha karibu mkuu. Nikampigia saluti kisha nikamsikia akisema Afande nashangaa sijapewa ripoti yoyote mpaka sasa mmefikia wapi upelelezi wenu.
Nikamjibu mkuu naomba mda kidogo niwaite wenzangu niwaulize wamefikia wapi kisha tukusanye taarifa kamili. Jioni ya leo nitakuja ofisini na majibu. Akaitikia sawa nawategemea sana Afande. Nikamjibu shaka ondoa mkuu. Akasema haya kazi njema. Alipoondoka nikawa. natafakari jinsi ya kujizuia na zile picha. Nikaona njia rahisi ni kuwaita maafande wenzangu wale wawili kisha nione kama wamepata hata viashiria vyovyote. Lengo ni kujua kama na mimi wamehisi kuhusika kwangu. Basi baada ya kumpigia simu Afande Peris na Afande Juma wakafika.
Kwa kua niliwazidi cheo walipofika wakanipigia saluti kisha wakaketi. Nikaanza kwa kuwauliza wamefikia wapi. Alianza Peris akasema Mkuu tulijaribu kufuatilia kwa kina sana na kwa karibu. Tulitumia baadhi ya mafaili ya majambazi sugu ili kuona kama tungeweza kupata uhusiano wa tukio na taarifa zao. Na kwa sasa tumefanikiwa kupata taarifa za watu wanne na taarifa zinaonyesha ushiriki wao katika tukio lile kwa namna mbalimbali. Mfano kuna huyu anaitwa Jarome singano, Huyu ni jambazi sugu na yeye ndiye alifadhili kikundi hiki kwa siraha na pesa.
Nilimkatisha kwa kusikia Jina lile la Jarome Singano kwani halikua geni katika kazi yangu. Nikamwuliza je huyu Jarome tunaweza kumpata? Afande inaonekana ana mtandao mkubwa sana. Mbaya zaidi inaonekana kuna vigogo wa serikalini wanashirikiana naye kwa ukaribu sana. Nikawajibu sawa tutajadili badae namna ya kumtia nguvuni na ni lazima atiwe nguvuni tuu. Haya na wa pili ni yupi?
Afande peris akaniangalia kisha akasema Mkuu huyu wa pili jina tumepata. Anaitwa Nurdin Kamisa jina maarufu "chinjachinja" Huyu alishiriki moja kwa moja katika tukio lile na tumebahatika kupata ushahidi wa picha ambao ni mkanda wa video. Huu unamwonyesha mshiriki akifyatua risasi ovyo eneo la benki. Akanikabidhi ule mkanda wa video. Afande Juma alikua kama kuna kitu anataka kusema. Nikamwuliza vipi afande kuna tatizo? Akasema ndio mkuu ni kuhusu wewe. Nilishtuka kiasi mana nikajua huenda naye amehisi nilishiriki kwani picha zangu sikuwaonyesha lakini huenda aliona yule mtu mwenye sura kama yangu kwenye ule mkanda. Nikajisemea moyoni kama ni hivyo nimekwisha. Kisha nikamwambia eenh sema ilo tatizo langu. Akanikazia macho kisha akasema.______________________
EmoticonEmoticon