MGOMO WA MAGARI MABOMU YARINDIMA STEND YA UBUNGO.

 


  Polisi Jijini Dar es Salaam wamelazimika kutumia mabomu ya machozi katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo kutuliza vurugu zinazofanywa na abiria pamoja na wananchi kufuatia mgomo wa madereva.

 Mgomo huo wa madereva wa mabasi na malori umeanza rasmi leo asubuhi nchi nzima na kuathiri kabisa sekta ya usafirishaji, ambapo Jijini Dar es Salaam mgomo huo pia umehusisha mabasi ya daladala.

Shuhuda wetu ameshuhudia katika neo la Ubungo bajaji na pikipiki nazo zinalazimishwa kugoma, Dereva akileta ubishi anapigwa na usafiri wake kuharibiwa.

 
Umati wa abiria wakiwa kwenye kituo cha daladala cha Darajani-Ubungo huku kukiwa hakuna daladala yoyote inayofanya kazi baada ya kutokea kwa mgomo wa madereva wa Daladala jijini Dar.
 
Baadhi ya abiria wakiwa wamepanda magari ya mizigo baada ya kukosekana kwa daladala maeneo yote ya jiji la Dar es Salaam leo asubuhi. 
Mmoja wa abiria akiongea na dereva wa kibasi kidogo kuangalia kama kuna uwezekano wa kupata usafiri maeneo ya Mwenge jijini Dar.
Katika kituo cha mabasi cha Mpakani eneo la Mwenge zilionekana Bajaj zikipakia na kushusha abiria baada ya madereva kuingia kwenye mgomo leo asubuhi.


Habari  toka  Morogoro  zinaarifu  kuwa  Abiria wamejazana  katika  vituo  vya  daladala, bodaboda ndo zinatoa msaada  (kwa wale wenye uwezo).

Previous
Next Post »