WAZIRI WA UCHUKUZI SAMUEL SITTA ASITISHA UINGIZAJI WA MABEHEWA 124 YALIYOBAKI TOKA NCHINI INDIA

WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesitisha uingizaji wa mabewa 124 yaliyobaki kutoka nchini India hadi atakapopata ripoti ya uchunguzi wa mabewa ya mizigo 150 yaliyochini utakapokamilika.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Sitta, alisema kama kuna watendaji wamefikia hatua ya kuingiza mabehewa yaliyochini ya kiwango basi hiyo ni sawa na hujuma.

Alisema kuwa uchunguzi wa mabehewa hayo 150 ulikuwa ukifanywa na Kamati Uchunguzi iliyoundwa na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Dk. Harrison Mwakyembe, unatarajiwa kukamilika siku ya Ijumaa Machi 13 mwaka huu.

“Waziri aliyenitangulia aliteua kamati kupitia Bodi nisema kuwa uwamuzi huu ni sahii na mimi na unga mkono kwani uamuzi huu  unatokana na ukweli kwamba mabehewa haya kuwa makuu hali inayosabisha mabehewa hayo kuwanguka kwa wastani wa Desemba mwaka jana yalikuwa yakianguka kila siku yawapo njiani hali inayosababisha hasara kwa nchi.

“Nimemuagiza Mwenyekiti wa Bodi Bodi ya TRL kukutana na Kamati ya uchunguzi siku ya Ijumaa ili kupitia taarifa hiyo na watakapomaliza wahakikishe kuwa hadi  Ijuma 16 iwe imenifikia ofisini kwangu ili kupata taarifa kamili kuhusu mabewa haya,”alisema Sitta.

Sitta alisema endapo taarifa ya uchunguzi huo itabainisha kuwa kulikuwa na ubabaishaji katika manunuzi ya mabehewa hayo 150, Serikali haita sita kuvunja mkataba  huo kwa kutumia sheria ya manunuzi.

Aliema licha ya kuvunja mkataba huo pia kunauwezekano mkubwa kumshitaki mhusika, kuaangalia kuwa ni nani mwingine amehusika kwenda kuangalia mabehewa hayo na kufikia hatua ya kupewa mabehewa hayo mabovu.

Alisema ikishindikana kuvunja mkataba huo basi itabidi wahusika walazimishwe kusimamia gharama za matengenezo ya mabehewa hayo ambayo tayari yamekwisha ingizwa nchi.

Sitta, alisema pia Serikali itaangalia ni nani alihusika kwenda kukagua kasha akakubali nchi ipate kitu kibovu, akibainika kutokana, uzembe huo na kuliletea hasara taifabasi ili aweze kuchukuliwa hatua za kisheri.

Aidha, alisema kuwa hali ya Shirika hili inazidi kuwa bora siku hadi siku hususani katika upande wa mapato.

Sitta, alisema katika kipindi cha Desemba mwaka jana, Shirika limeweza kuzalisha kiwango cha dola za kimarekani 140 ukilinganisha na kiwango cha dola 30 Junuari huo huo, ambacho hicho ndio cha chini kabisa.

“Pia tumepata taarifa kuwa hali ya usafiri wa abiria unazidi kuimarika kwani hivi sasa kuna vichwa 60 ambapo mahitaji ni vichwa 107 lakini kwa kuwa na hivi hali si mbaya,”alisema Sitta.

Akizungumzia kuhusu watumishi, Sitta, alisema watumishi wanapaswa kulipwa kama mikataba yao inavyoonesha katika makubaliano yao.
Previous
Next Post »